Nenda kwa yaliyomo

Volkswagen

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Volkswagen Group)
Volkswagen logo 2019-present
Kiwanda cha viwanda cha Volkswagen huko Wolfsburg, kilichoonyeshwa mnamo 2006
Nchi penye viwanda vya makampuni chini ya VW duniani

Volkswagen (maana ya Kijerumani: gari la wananchi) inayojulikana pia kwa kifupi chake VW (tamka ing. vii-dabl-yu au jer. vau-we) ni kampuni ya kutengeneza motokaa kutoka nchini Ujerumani. Makao makuu yapo mjini Wolfsburg katika jimbo la Saksonia Chini lakini ina viwanda katika sehemu nyingi za Ujerumani na nchi nyingi hadi Afrika, Asia na Amerika.

Kampuni ya Volkswagen ni pia mwenye makampuni ya Audi, Bentley, Bugatti, Lamborghini, Seat, Škoda na Scania. Ni kampuni kubwa ya kutengeneza magari katika Ulaya na ya tatu duniani. Imetangaza ya kwamba inalenga kuwa kampuni kubwa ya kutengeneza magari duniani kabisa.

Takwimu za biashara

[hariri | hariri chanzo]
Mwaka Mapato
milioni Euro
Mapato
baada ya kulipa kodi
milioni Euro
Magari yaliyotengenezwa
milioni
Wafanyakazi
(wastani ya mwaka)
elfu
1972 8,180 (15,999 Mio, DM) (haijulikani) (haijulikani) 192
1990 34,800 (68,063 Mio, DM) (haijulikani) (haijulikani) 261
1997 57,800 (113,047 Mio, DM) (haijulikani) (haijulikani) 280
2000 81,840 (160,065 Mio, DM) 2,610 5.165 322
2001 87,300 (170,744 Mio, DM) 2,930 5.107 324
2002 85,293 2,597 4.984 324
2003 84,813 1,003 5.016 335
2004 88,963 697 5.079 343
2005 93,996 1,120 5.243 345
2006 104,875 2,750 5.734 324.9
2007 108,897 4,122 6.192 329.3 (+1.1 %)
2008 113,808 4,688 6.272 369.9 (+12.3 %)
2009 105,187 911 6.310 368.5 (-0.4 %)

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Chanzo cha kampuni ilikuwa mnamo mwaka 1937. Wakati ule dikteta wa Ujerumani Adolf Hitler alitaka motokaa yenye bei nafuu kwa wananchi wa kawaida na "Volkswagen" ina maana ya "gari la wananchi" iliyoweza kubeba familia ya watu 4 na kutembea kwa mkasi wa 100 km/h. Muhandis Ferdinand Porsche aliombwa kutunga gari lenye bei ndogo lililoweza kupatikana kwa watu wengi wenye mishahara midogo. Kutokana na umbo lake limejulikana kwa jina la "Käfer" (ing. beetle yaani mdudu mwenye umbo la kangambili). Kiwanda kipya kilianzishwa mashambani karibu la boma la kale lililoitwa "Wolfsburg" likawa chanzo cha mji wa baadaye. Kiwanda kilikamilishwa mwaka 1939 miezi michache kabla ya mwazo wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Kutokana na vita magari yaliyokusudiwa hayakujengwa badala yake modeli zilibadilishwa kwa matumizi ya kijeshi. Baada ya kushindwa kwa Ujerumani Wolfsburh ilikuwa chini ya utawala wa Kiingereza kwa miaka 4 na Waingereza walisita kwa muda kama wangeendeleza kiwanda au kuiuza. Lakini waliona modeli ya Volkswagen iliyoanza kutolewa sasa kwa idadi ndogo haikufaa waliwachia Wajerumani. Lakini katika miaka iliyofuata tangu Ujerumani ya Magharibi ilirudishwa hali ya kujitawala gari lilelile likawa ishara ya kurudishwa kwa nguvu ya kiuchumi. Mwaka 1955 tayari milioni 1 ya motokaa zenye umbo la dudu zilitembea barabarani. Mafanikio ya kampuni yaliendelea kwa kutoa modeli mpya na kubwa zaidi. Mnamo 1965 VW ilinunua kiwanda cha NSU - Audi na kampuni hii ilibuni aina za modeli kama Golf na Passat zilizouzwa baadaye tangu 1974 kama kizazi kipya cha VW baada ya mauzo ya VW-beetle kupungua. Model ya zamani iliendelea kutengenezwa katika viwanda huko Meksiko na Brazil.

Tangu 1986 VW iliendelea kunua makampuni mengine kama Seat ya Hispania, Skoda ya Ucheki na mengine. VW imeendelea kupanusha utengenezi wake hata nje ya magari ya familia. Siku hizi jumuiya ya makampuni chini ya VW inatengeneza magari ya mizigo, malori, magari ya michezo, magari yenye bei za juu na mengine.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Volkswagen kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.