Nenda kwa yaliyomo

Lamborghini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lamborghini likiwa barabarani.

Lamborghini ni gari lenye bei kubwa sana, na lina thamani ya Dola 200,000, ambayo ni sawa na shilingi za Kitanzania 449,060,000. Gari hili pia linasifika kuwa ni gari lenye spidi kubwa, kwani gari hili linasafiri kwa kilometa 350 kwa saa, na linashika nafasi ya 10 kwa magari yenye spidi kubwa sana duniani.

Automobili Lamborghini ni kiwanda cha Italia ambacho ni mtengenezaji wa magari ya fahari, magari ya michezo na SUVs kinachopatikana Sant'Agata Bolognese, Italia.

Kampuni hiyo inamilikiwa na kundi la Volkswagen kupitia hisa za magari ya Audi.

Kampuni hiyo imekadiriwa itakuwa na hasara ya kila mwaka ya $ 450 milioni ifikapo 2030.