Visensya Gerosa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Visensya Gerosa akifanya utume wake.

Visensya Gerosa, kwa Kiitalia Vincenza Gerosa, (29 Oktoba 178420 Juni 1847) alikuwa mwanamke wa Italia kaskazini ambaye, pamoja na Bartolomea Capitanio, alianzisha shirika la Masista wa Upendo wa Lovere, ambao kwa kawaida wanaitwa Masista wa mtoto Maria.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Visensya alizaliwa katika kijiji hicho cha Lovere, mkoani Lombardia, katika familia tajiri. Jina lake la awali lilikuwa Caterina.

Alikutana na Bartolomea alipokuwa na umri wa miaka 40 years, wakaungana kupambana na ujinga na ufukara wa watu wa eneo lao.

Baada ya Bartolomea kufariki, Visensya aliendeleza shirika lao kwa miaka mingi akafariki mwaka 1847 hukohuko Lovere.

Wote wawili walitangazwa wenye heri na Papa Pius XI tarehe 30 Mei 1926, halafu watakatifu na Papa Pius XII tarehe 18 Mei 1950.

Sikukuu ya Visensya inaadhimishwa kila mwaka tarehe 28 Juni[1].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Attwater, Donald (1993). The Penguin Dictionary of Saints, 3rd, New York: Penguin Books. ISBN 0140513124. 
  • G. Lubich, P. Lazzarin, Vincenza Gerosa, la ”sciura” della carità, Città Nuova, 1982

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.