Bartolomea Capitanio

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Bartolomea Capitanio (13 Januari 1807 - 26 Julai 1833) alikuwa mwanamke wa Italia kaskazini ambaye, pamoja na Visensya Gerosa, alianzisha shirika la Masista wa Upendo wa Lovere, ambao kwa kawaida wanaitwa Masista wa mtoto Maria.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Bartolomea alizaliwa katika kijiji hicho cha Lovere, mkoani Lombardia.

Alipokutana na Visensya waliungana kupambana na ujinga na ufukara wa watu wa eneo lao.

Mwaka 1833 walisaini hati ya kuanzisha shirika, lakini baada ya miezi tu alifariki.

Hata hivyo Visensya aliendeleza shirika lao kwa miaka mingi akafariki mwaka 1847 hukohuko Lovere.

Wote wawili walitangazwa wenye heri na Papa Pius XI tarehe 30 Mei 1926, halafu watakatifu na Papa Pius XII tarehe 18 Mei 1950.

Sikukuu ya Bartolomea inaadhimishwa kila mwaka tarehe 26 Julai.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Attwater, Donald (1993). The Penguin Dictionary of Saints, 3rd, New York: Penguin Books. ISBN 0140513124. 
  • G. Lubich, P. Lazzarin, Bartolomea Capitanio, una possibile compagna di viaggio, Città Nuova, 1982

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bartolomea Capitanio kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.