Nenda kwa yaliyomo

Uvuvi nchini Angola

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Uvuvi Nchini Angola)
Wavuvi nchini Angola
Wavuvi nchini Angola

Uvuvi nchini Angola mara nyingi hufanya na wavuvi wa Kigeni. Baadhi ya wavuvi hawa wanaotumia maji ya Angola walitakiwa na serikali kuacha baadhi ya samaki nchini Angola ili kuongeza usambazaji wa samaki nchini humo. Mapatano kama haya ya uvuvi yaliafikiwa na nchi kama Uhispania, Japani na Italia.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Uvuvi nvhini Angola ulikuwa nyanja kuu ya uchumi na iliyoendelea kukua kabla ya Uhuu kutoka kwa Wareno mnamo 1975. katika miaka ya mwanzo ya 1970s, kulikuwa na mashua takribani 700 ya kuvua samaki.

Pato la kila mwaka la samaki lilikuwa zaidi ya tani 300,000. Ikijumuishwa na uvuvi wa kigeni kutoka eneo lililotawaliwa na Ureno la Angola, pato lote lilikuwa zaidi ya tani miliono moja. Namibe|Moçâmedes]] pamoja na Luanda, Benguela na Lobito zilikuwa bandari kuu za uvuvi.

Kufuatia uhuru mnamo 1980, uvuvi wa Angola uliianza kuporomoka kufuatia kutoroka kwa Wavuvi wa Kirenowaliokuwa na uchuzi. Baada ya Mapinduzi ya Kijeshi ya Lisbon mnamo Aprili 1974, Angola kama mkoa mmoja wapo wa nje wa Ureno ilianza kudidimia kiutawala na uhuru ulibidi. Mashua nyingi za uvuvi ziliondoka kwenda Ureno pamoja na wavuvi na familia zao.kufikia 1986, ni 70 juu ya mashua za kuvua 143 zilikuwa zikindelea nchini Namibe, bandari iliyokuwa ikitoa karibu thuluti mbili za samaki. Isitoshe viwanda vingi vya samaki vilikuwa vikiitaji kufanyiwa marekebisho. Angola mbayo ilikuwa mwuuzaji wa nje wa samaki sasa haingeweza kujitosheleza

Hii inamaanisha kuwa serikali iliyakubalia mataifa kuuza pato lao lote kwao oli kupata fedha za leseni.

Miaka ya kati ya 1980, serikali ilianza kuifufua sekta ya uvuvi hasa katika maeneo ya Mkoa wa Namibe na a wa Benguela. Jukumu lililopewa kipaumbele ni urekebishaji wa mashine zilizozeeka za kuvua.Ili kufikia lengo hili, seikali ilipokea usaidizi kwa nchi za nje. Mnamo 1987 EEC ilitangaza mipango yake ya kutoa pesa kusaidia katika kujenga tena maeneo ya kuegeza meli ya Dack Doy na viwanda viwili vya kupika samaki mjini Tombua. ispania iliiuzia Angola mashua za kuvua 27 za chuma za thamani ya US$ miliono 70, na mashua 14 za kisasa ziliahidiwa kutoka Italia-

Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uvuvi nchini Angola kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.