Muziki wa Angola

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Muziki wa Angola umejengeka kutokana na matukio mengi ya kimuziki na kisiasa katika historia ya nchi hiyo. Katika karne ya 20, Angola imekumbwa na ghasia na vurumai za kisiasa. Wanamuziki wake wamedhulumiwa na Serikali wakati wa Ukoloni na Baada ya Ukoloni. Muziki wa Angola pia ulishawishi muziki wa Lusophone nchini Brazil na Ule wa Cuba.

Miondoko[hariri | hariri chanzo]

Mji mkuu wa Angola ni Luanda ambao una sampuli tofauti tofauti za midundo ikiwemo merengwe, kilapanda na semba, ya mwisho ikiwa mwondoko ambao unashirikisha Roots na Samba ya Brazil zikiwekwa pamoja. Katika pwani ya Luanda pia kuna nji wa Ilha do Cabo, ambao umetawalwa na muziki unaotumia vyombo vya accordion na harmonica. Mwondoko unaitwa rebita.

Umaarufu wa Kimataifa[hariri | hariri chanzo]

Ikilinganishwa na nchi jirani za kusini mwa Afrika na koloni zingine za Ureno, Angola ndiyo iliyo na umaarufu mkuu zaidi kimataifa.

Kundi la kwanza kujulikana nje ya Angola lilikuwa Orquestra os Jovens do Prenda, ambalo lilikuwa maarufu katika miaka ya 1960 hadi mapema 1970s na wameendelea kutumbuiza na kurekodi tangu hapo. Bendi kuu ilishirikisha Trumphet mbili, Saksafoni moja, Guitar nne na nusu dazani ya vyombo vya Percussion. Walicheza kizomba, mwondoko wa kiasili ambao unajengeka na marimba au xylophone huku wakitumia gitaa nne kulinganisha na sauti ya marimba na quilapanga.

Miondoko ya Pop[hariri | hariri chanzo]

Miaka ya 1950 hadi 1960[hariri | hariri chanzo]

Carlos Vieira Dias, mchezaji wa gitaa ya akostiki, hata hivyo, ndiye mwanzilishi wa miondoko ya Pop nchini Angola. Alianzisha sauti za ensemble za dikanza (scraper, ngomas (conga drums) na viola, ambazo zilikuwa maarufu miaka ya 1950 katika mitaa ambapo watu walipenda ujumbe uliotiwa mawazo ya siasa na ushujaa a kutaifa. Dias alifungwa na Wareno kwa miaka mingi


Punde baada ya Vita nchini Angola, Mwondoko wa Rock ulitamba nchini. Msanii mmoja katika kundi maarufu alilinaganisha katika kundi maarufu na kuwa katika timu mashughuli ya Soka, wakati bendi yake iliingia kwa mkahawa wake walimshangilia (na makundi shindani yangewasinya).[1].

Miaka ya 1970[hariri | hariri chanzo]

Kuanzia miaka ya 1970 mwanamuziki Bonga alijulikana zaidi katika miondoko ya Pop zaidi wa Angola. Alianza kutumbuiza mapema miaka ya 1960 wakati muziki wa kiasili (Folk) wa Angola ulikuwa ukipata umaarufu. Kama mwanachama wa kundi la Kissueia, alijishughulisha na shida za kijamii za watu wakati huo huo akiwa sogora wa Soka. Aliamishwa na serikali ya Kikoloni kwenda Lisbon ambapo alicheza soka hadi 1972 aliporejea kupinga utawala wa kikoloni nchini Angola. Alihamia Rotterdam, ambapo alijihusisha kwa karibu na jamii ya Cape Verde. Wimbo wake wa "Mona Ki Ngi Xica" (1972) ulimpa kibali cha kutiwa nguvuni na akaanza kutembelea Ujerumani, Ufaransa na Ubelgiji hadi Angola ilipopata uhuru mnamo 1975.

Miaka ya 1980[hariri | hariri chanzo]

Mapema miaka ya themanini, Muziki wa Pop wa Angola ulishawishiwa vikali na Muziki wa Cuba, hasa katika kazi ya André Mingas. Rumba ya Cuba ilikuwa maarufu nay a ushawishi mkuu Kusini mwa Afrika zikiwemo nchi jirani za Zaire, ambapo ilijiimarisha kama msingi wa mwondoko wa soukous. Kando na kuenea kwa muziki wa Cuba uliorekodiwa, majeshi ya Cuba ambayo yaliungana na MPLA ya Angola yalisaidia kueneza modundo ya Cuba nchini.

Maneno ya ngoma hizi yameandikwa kwa Lugha ya Kireno ambayo huzungumza na watu wengi nchini Angola kama lugha ya kwanza nay a Pili kando na Lugha za Kibantu

Wanamuziki wengine maarufu wa Angola ni pamoja na Teta Lando, Carlos Lamartine, Kituxi, Waldemar Bastos na Afra Sound Star.

Kwa muda sasa, muziki wa aina mpya ambayo kwa ukubwa inashirikisha vifaa vya elektroniki ambao unaitwa kuduro, umechipuka nchini Angola.

Tazama Pia[hariri | hariri chanzo]


Virejeleo[hariri | hariri chanzo]

  • Hyde, Christian and Richard Trillo. "Struggle and Talent". 2000. In Broughton, Simon and Ellingham, Mark with McConnachie, James and Duane, Orla (Ed.), World Music, Vol. 1: Africa, Europe and the Middle East, pp 428-431. Rough Guides Ltd, Penguin Books. ISBN 1-85828-636-0
  • Moorman, Marissa "Intonations: A Social History of Music and Nation in Luanda, Angola, from 1945 to Recent Times" Ohio Univ Press 2008[1]