Nenda kwa yaliyomo

Usubi (Ceratopogonidae)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Usubi
Usubi akifyonza damu (Culicoides impunctatus)
Usubi akifyonza damu (Culicoides impunctatus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Diptera (Wadudu wenye mabawa mawili tu)
Nusuoda: Nematocera (Diptera wenye vipapasio vifupi)
Familia ya juu: Chironomoidea
Familia: Ceratopogonidae
Newman, 1834
Ngazi za chini

Nusufamilia 5:

Usubi (pia visubi) ni mbu wadogo wa familia Ceratopogonidae katika oda Diptera wanaofyonza damu. Spishi nyingi hueneza magonjwa kama vile mansoneliasisi, ugonjwa wa ulimi buluu na ugonjwa wa farasi wa Afrika. Kuna visubi wengine walio wana wa nusufamilia Phlebotominae katika familia Psychodidae. Visubi hao hufyonza damu pia na kueneza magonjwa. Halafu kuna visubi weusi wa familia Simuliidae ambao hueneza upofu wa mtoni.

Mbu hawa ni wadogo sana, mm 1-5. Rangi yao ni kijivu, hudhurungi, kahawia au kahawianyekundu. Macho ni meusi kwa kawaida. Mara nyingi toraksi (kidari) imepindika na kwa hivyo kichwa kinaelekea chini.

Chakula cha usubi ni mbochi, lakini majike wanahitaji damu ya mamalia, ndege au reptilia ili mayai yaendelee. Spishi fulani hufyonza “damu” ya wadudu wengine.

Usubi wengi, spishi za jenasi Culicoides hasa, ni vekta za magonjwa mbalimbali kama vile mansoneliasisi, ugonjwa wa ulimi buluu, ugonjwa wa farasi wa Afrika na virusi nyingi nyingine. Vekta ya ulimi buluu katika Afrika ya Mashariki ni Culicoides pallidipennis na labda C. cornutus, C. grahami, C. magnus na C. tororoensis pia.

Spishi kadhaa za Afrika ya Mashariki

[hariri | hariri chanzo]
  • Culicoides imicola
  • Culicoides nairobiensis
  • Culicoides pallidipennis
  • Culicoides schultzei