Urundi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Jina la "Urundi" kwenye ramani ya kikoloni (1929)

Urundi (kwa tahajia ya Kifaransa pia Ouroundi) ni jina la kihistoria kwa nchi ya Burundi. Wajerumani waliita nchi "Urundi" walipoanza kueneza utawala wao juu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani wakaitawala kwa njia ya . Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia eneo hili lilivamiwa na jeshi la Ubelgiji kutoka koloni ya Kongo ya Kibelgiji na kuwa eneo la kudhaminiwa chini Ubelgiji baadaye. Wabalgiji wakaitawala pamoja na Rwanda kwa jina la "Ruanda-Urundi" hadi uhuru kwenye mwaka 1962 na tangu wakati ule nchi inaitwa rasmi "Burundi".

Inaonekana ya kwamba Wajerumani walipoanza kutumia umbo la "Urundi" walifuata kawaida ya lugha ya Kiswahili badala ya jina la wenyewe ambako silabi kwa mahali ni "Bu-" si "U-" jinsi ilivyo kwa Kiswahili.