Ulrike Lohmann
Ulrike Lohmann ni mtafiti wa hali ya hewa na profesa wa fizikia ya anga katika ETH Zurich. Ulrike Lohmann anafahamika kutokana na utafiti wake wa chembe za aerosol kwenye mawingu.
Maisha Ya Awali, Elimu Na Kazi
[hariri | hariri chanzo]Alitokea Kiel kama binti wa mwalimu na mwanasiasa katika Chama cha Kijamaa cha Kidemokrasia cha Ujerumani [1]. Lohmann alijitolea kwa mwaka mmoja katika kijiji cha watoto cha SOS nchini Nigeria, kisha akasomea etnolojia na jiografia. Ulrike Lohman alichochewa na ripoti za mazingira kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, alisomea meteorolojia katika Chuo Kikuu cha Mainz kuanzia mwaka 1988 hadi 1993[1][2].Lohmann alipokea udaktari wa hali ya hewa katika Taasisi ya Max Planck mwaka 1996[3].
Awali, alifanya kazi kama msaidizi wa profesa na profesa msaidizi wa sayansi ya angahewa katika Chuo Kikuu cha Dalhousie[2] [2]. Tangu mwaka 2004, amekuwa profesa kamili wa fizikia ya angahewa katika Taasisi ya Angahewa na Hali ya Hewa ETH Zurich[2]
Maisha binafsi
[hariri | hariri chanzo]Lohmann anaishi katika ziwa la Zurich na shauku yake ni michezo ya uvumilivu na kuogelea.
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]- Tuzo Ya Mwanachama aliyechaguliwa, Chuo cha Kitaifa cha Sayansi cha Ujerumani, Leopoldina(2014).
- Shahada ya heshima ya udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Stockholm (2018).
- Golden Tricycle kutoka ETH Zurich kwa uongozi unaofaa kwa familia (2013).
- Mwanachama aliyechaguliwa, Chuo Kikuu cha Sayansi ya Kitaifa cha Ujerumani, Leopoldina (2014).
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 "Die Wolkenfrau", Der Bund, August 31, 2019. (de)
- ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 Switzerl, Address ETH Zürich Dep of Environmental Systems Science Prof Dr Ulrike Lohmann Institut für Atmosphäre und Klima CHN O. 11 Universitätstrasse 16 8092 Zürich. "Lohmann, Ulrike, Prof. Dr. | ETH Zurich". usys.ethz.ch (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 10 Septemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: numeric names: authors list (link) - ↑ Kigezo:Cite thesis