Nenda kwa yaliyomo

Tunde Nightingale

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Honest Olatunde Thomas (10 Desemba 1922 - 1981) anajulikana kama Tunde Nightingale au The Western Nightingale, alikuwa mwimbaji na mpiga gitaa wa nchini Nigeria. Tunde anajulikana sana kwa mtindo wake wa kipekee wa muziki wa jùjú.[1]

Alizaliwa mjini Ibadan, akasoma shule katika mji wa Lagos, akahudumu katika jeshi na kufanya kazi katika kampuni ya reli.[2] Alianzisha kikundi chake cha kwanza cha bendi kinachojulikana kwa jina la three piece band kikiwa na gitaa, tari na shekere mnamo mwaka 1944.[3] Hii ilikuwa mwanzo wa kipindi wanamuziki wa Nigeria walianza kutumia gitaa kama sehemu ya rekodi zao za muziki. Lakini mtindo wake wa muziki wa juju haukuwa maarufu sana miongoni mwa wasomi wa Lagos. Mwaka 1952 bendi yake chini ya jina la Tunde Nightingale na bendi yake ya Agba Jolly Orchestra walikua wakifanya maonyesho ya mara kwa mara katika Klabu za Afrika Magharibi, Ibadan. Kikundi chake kiliwajumuisha waimbaji Ayinde Bakare, I. K. Dairo na Dele Ojo. Mnamo mwaka 1952 kikundi chake kiliongeza wanachama hadi kufikia wanachama nane na kucheza katika west African club huko Ibadan. Kati ya mwaka 1954 na 1964 Nightingale alipata umaarufu kwa kiasi kikubwa ingawa hakua na nyimbo nyingi. Katikati ya mwaka 1960 alisaini mkataba na Mr. Jossy Fajimolu ilikuwa ni katika kipindi muziki wake ulipata umaarufu miongoni mwa baadhi ya wanajamii wa mjini Lagos ambao waliona muziki unafaa zaidi kwa ajili ya vyama vya kijamii kuliko kumbi za dansi. Mnamo mwaka 1960 umaarufu wake ulikuwa umekua katika jamii za Lagos ambazo zilimdhamini kwa ziara ya nje aliporudi alijiunga na lebo ya TYC. Kwa ujumla alirekodi albamu zaidi ya 40 katika wasifu wake.[4]

  1. Waterman, Christopher Alan (1990). Juju: A Social History and Ethnography of an African Popular Music. University of Chicago Press. ku. 110–112. ISBN 0226874656.
  2. Daramola, Dapo (Julai 1967). "So Wan be Spreads like Wildfire". Drum Magazine (Lagos). Lagos: Drum Publications.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Omojola, Bode (2012). Yorùbá Music in the Twentieth Century: Identity, Agency, and Performance Practice. University of Rochester Press. uk. 166. ISBN 978-1580464093.
  4. "TUNDE NIGHTINGALE: A LEGEND FOR ALL TIMES". African Songs UK. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-06-07. Iliwekwa mnamo 2009-11-02.
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tunde Nightingale kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.