Treni ya umeme
Treni ya umeme ni tofauti na treni nyingine zinazotumia mafuta ili kuweza kutembea.Treni ya umeme hutumia nishati ya umeme kutembea kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa haraka sana, tofauti na treni za mafuta.
Treni hizi za umeme hubeba abiria tu na kwenda kwa mwendo kasi wa zaidi ya kilomita mia tatu kwa saa moja. Pia kuna kiyoyozi kizuri kwa ajili ya kuweka baridi ndani ya treni kwani madirisha ya treni hii huwa hayafunguki.
Ndani mna huduma mbalimbali kama vile huduma za chakula na vinywaji, huduma ya mapumziko yaani kulala, hata huduma ya mtandao. Huduma hii ya mtandao huwawezesha abiria kujua mambo mbalimbali yanayoendelea sehemu mbalimbali wakiwa katika chombo hiki tofauti na abiria wanaokuwa katika treni ya kawaida inayotoa moshi.
Treni ya aina hii inatumika sana katika nchi zilizoendelea, kwa mfano Ujerumani, Marekani, na nchi kadhaa barani Afrika kama vile Ethiopia, Kenya na Afrika ya Kusini. Ukiaangalia maendeleo ya nchi hizi ni mazuri kutokana na msaada wa treni ya umeme kusafirisha watu kwa haraka katika maeneo yao ya kazi.
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |