Kiyoyozi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kiyoyozi juu ya dari la nyumba.
viyoyozi nje ya jengo

Kiyoyozi ni kifaa kinachowekwa kwenye vyombo vya moto au nyumba. Kifaa hiki kina uwezo wa kutoa hewa ya ubaridi au ya joto.

Kwa sehemu zenye joto watu hutumia kifaa hiki kufanya hali ya hewa kuwa yenye ubaridi katika nyumba zao au katika magari yao na vyombo vinginevyo vya moto kama vile treni.

Kumbe katika sehemu zenye baridi watu hutumia kifaa hiki kufanya hali ya hewa katika nyumba zao au magari yao kuwa ya joto la kawaida ili kujikinga na baridi kali.

Kwa sasa kifaa hiki kinatumiwa na watu wengi hasa katika nchi zilizoendelea.

Kifaa hiki kinatumia umeme mwingi, hivyo kinahitaji umeme wa kutosha ili kufanya kazi yake.