Nenda kwa yaliyomo

Tenzi tatu za kale

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Tenzi tatu za kale ni kitabu cha historia kinachoelezea tenzi tatu zilizoandikwa katika karne 14 hadi mwanzoni mwa karne ya 19 [1]

Kitabu hicho kimeelezea hali ya kihistoria ya kisiasa katika pwani ya Afrika ya Mashariki kikielezea jinsi siasa zilivyokuwa katika miji ya Pate na kugusia maeneo mengine kama visiwa vya Zanzibar na kuzungumzia maisha ya watawala wakubwa waliokuwepo katika karne hizo Sayyid Mansab na tawala nyingine za Kiomani mwaka 1730 hadi 1890.

Ndani ya kitabu hicho, zimeelezwa pia tenzi za kale zaidi ambazo ni Utendi wa Fumo Liyongo, Utenzi wa Mwanakupona na Utenzi wa inkishafi; tenzi hizo zinaweza kutumika kama sehemu ya historia ya miji katika Afrika ya Mashariki katika mambo ya lugha na sanaa ya ushairi [2]

Ndani ya kitabu hicho unapatikana pia wimbo maarufu ulioandikwa na Fumo Liyongo ujulikanao kama Wimbo wa Kijakazi Saada.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Tenzi tatu za kale. Mulokozi, M. M. (Mugyabuso M.), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. Dar es Salaaam: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. 1999. ISBN 9976-911-34-3. OCLC 45248518.{{cite book}}: CS1 maint: others (link)
  2. "UCHAMBUZI WA TENDI TATU ZA KALE – Mwalimu Wa Kiswahili" (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-02-19. Iliwekwa mnamo 2020-02-19.
Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tenzi tatu za kale kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.