Tenno

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Tenno Akihito mwaka 2005

Tenno ni cheo cha mfalme au kaisari wa Japani. Kufuatana na katiba ya nchi yeye ni "ishara wa dola na wa umoja wa taifa".

Tenno wa sasa ni Akihito aliyepokea cheo baada ya kifo cha babake Hirohito mwaka 1989.

Historia ya Japani inamkumbuka tenno wa kwanza kabisa aliyekuwa Jimmu mnamo 660 KK. Wataalamu wengine huwa na mashaka lakini wanakubali ya kwamba watawala hawa walikuwepo angalau tangu karne ya 5 BK. Hadi karne ya 19 ikulu yao ilikuwa mjini Kyoto, tangu Meiji iko Tokyo.

Nasaba ya watawala wa Japani ni nasaba ya kale duniani.

Katika historia ndefu matenno walikuwa na madaraka tofautitofauti. Hata kama walitazamiwa kama wakuu wa taifa hali halisi madaraka yao yalikuwa madogo wakati mwingine. Lakini kulikuwa pia na matenno walioamua kabisa juu ya siasa ya nchi kwa mfano Meiji tangu 1868.