Nenda kwa yaliyomo

Daraja la Mfugale

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Tazara Flyover)
Muonekano wa Tazara Flyover kwa upande wa duka la Azam Ice Cream.

Daraja la Mfugale (vilevile: Flyover ya Tazara, Daraja la Tazara, Barabara ya Juu ya Tazara) ni daraja linalorahisisha mwendo wa magari kwenye njiapanda ya Barabara ya Nelson Mandela na Barabara ya Julius K. Nyerere, karibu na stesheni kuu ya reli ya TAZARA jijini Dar es Salaam, Tanzania. Jina la Mfugale liliteuliwa kwa heshima ya mhandisi kiongozi na mkurugenzi wa mamlaka ya TANROADS,Patrick Mfugale [1].

Hii ndiyo flyoover ya kwanza nchini Tanzania. Mnamo tarehe 15 Septemba 2018 daraja limeanza kutumika rasmi. Lilijengwa kwa msaada kutoka nchi ya Japani na kujengwa na kampuni ya ujenzi kutoka hukohuko Japani maarufu kama "Sumitomo Mitsui Construction Co., Ltd. (SMCC)."[2]

Daraja lipo chini ya wakala wa barabara Tanzania, TANROADS. Mkataba kati ya Tanzania National Roads Agency (TANROADS) na Sumitomo Mitsui Construction Co.,Ltd. (SMCC) ulisainiwa mnamo tarehe 15 Oktoba, 2015. Lengo likiwa kuboresha makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela. Mradi huu ulifadhiliwa na Japan International Cooperation Agency (JICA).

JICA, na washika dau wengine ikiwa ni pamoja na wakazi wa Dar es Salaam na Tanzania nzima, walikuwa wakisubiria kwa hamu ujenzi wa daraja hili. Serikali ya Japan, kupitia wakala wake JICA, ina historia ndefu ya zaidi ya miaka 30 imekuwa ikisaidia miundombinu mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, tangu walivyojenga daraja la Selander mnamo mwaka wa 1980.[2]

Ujenzi ulianza mapema mnamo mwezi Machi 2016 na mnamo tarehe 16 Aprili 2016, Rais John Pombe Magufuli alizindua ujenzi wa daraja hilo.[3][4][5]

Mnamo tarehe 15 Septemba 2018 daraja limeanza kutumika rasmi, huku likiacha mambo machache tu ili kukamilisha ujenzi wake. Makubaliano ya kumaliza daraja la Tazara ni Oktoba 2018.

Picha

Marejeo

  1. Hundrds attend Tazara flyover launch, tovuti ya gazeti The Citizen (Tanzania), 27-09-2018
  2. 2.0 2.1 "Tazara Flyover Construction is starting | Tanzania | Countries & Regions | JICA". www.jica.go.jp (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-01-26. Iliwekwa mnamo 2018-09-15.
  3. "Magufuli azindua ujenzi wa 'fly over' Tazara DSM | East Africa Television". www.eatv.tv (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2018-09-15.
  4. "Rais Magufuli Azindua Mradi wa Barabara ya Flyover -Tazara - Global Publishers", Global Publishers (kwa American English), 2016-04-16, iliwekwa mnamo 2018-09-15
  5. "Magufuli azindua flyover, atema cheche", Mwananchi (kwa Kiingereza), 2016-04-17, iliwekwa mnamo 2018-09-15

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons