Kalonzo Musyoka

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Stephen Kalonzo Musyoka)
Jump to navigation Jump to search
Picha ya Dr.Kalonzo Musyoka

Stephen Kalonzo Musyoka (* 24 Desemba 1953 kijijini Tseikuru katika wilaya ya Mwingi) ni mwanasiasa nchini Kenya kutoka Ukambani.

Mwanasiasa wa KANU[hariri | hariri chanzo]

Alijiunga na siasa katika chama cha KANU akachaguliwa kuwa mbunge mara ya kwanza 1985 katika uchaguzi mdogo wa Kitui-North (baadaye Mwingi-North). 1986 alipewa kazi ya waziri msaidizi katika wizara ya kazi za umma.

Waziri wa mambo ya Nje[hariri | hariri chanzo]

Akarudi bungeni 1988 akachaguliwa kuwa naibu spika wa bunge. Baada ya kuchaguliwa tena 1992 alikuwa waziri wa mambo ya nje akaendlea kushika ofisi hii hado 1998 alipohamishwa kwenda wizara ya elimu halafu ya utalii.

Kujiunga na LDP na NARC[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya uchaguzi wa 2002 alijiunga na kundi la Raila Odinga lililondoka katika KANU baada ya uteuzi wa Uhuru Kenyatta kuwa mgombea wa uraisi kwa chama hiki akajiunga katika LDP.

Baada ya ushindi wa NARC katika Desemba 2002 alirudishwa 2003 kama waziri wa mambo ya nje chini ya rais Mwai Kibaki. Katika mabadiliko ya serikali kutokana na mafarakano ya kwanza katika NARC alihamishwa 2004 wizara wizara ya mazingira na maliasili hadi 2005.

Serikali ilipovunjwa 2005 na rais baada ya kura maalumu ya wananchi juu ya katiba ya Kenya Kalonzo pamoja na mawaziri wengi wa LDP hakurudishwa serikalini. Alishiriki katika umoja wa upinzani kwenye "kambi la machungwa".

Mgombea wa urais 2007[hariri | hariri chanzo]

Musyoka alikuwa kati ya viongozi wa Orange Democratic Movement hadi farakano kuhusu uongozi kabla ya uchaguzi wa 2007. Musyoka alifaulu kushika chama asilia cha ODM-Kenya kilichoomteua kama mgombea wa urais.

Katika uchaguzi wa rais wa desemba 2007 alipata nafasi ya tatu baada ya Kibaki na Odinga akichukua karibu asilimia 10 za kura kitaifa. Chama chake cha ODM-Kenya kilishinda jumla viti 15 bungeni hasa viti 13 kati ya 17 vya Ukambani.

Kuingia katika serikali ya pili ya Kibaki[hariri | hariri chanzo]

Tar. 08-01-2008 Musyoka alitangazwa kama makamu wa rais.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: