Space Jam
Space Jam | |
---|---|
Imeongozwa na | Joe Pytka |
Imetayarishwa na | Ivan Reitman Joe Medjuck Daniel Goldberg |
Imetungwa na | Leo Benvenuti Steve Rudnick Timothy Harris Herschel Weingrod |
Nyota | Michael Jordan Bugs Bunny Wayne Knight Daffy Duck Lola Bunny Theresa Randle Bill Murray |
Muziki na | James Newton Howard |
Imesambazwa na | Warner Bros. |
Imetolewa tar. | 15 Novemba 1996 (Marekani) |
Ina muda wa dk. | Dakika 88 |
Lugha | Kiingereza |
Bajeti ya filamu | Dola za US. 80,000,000 US (makadirio) |
Mapato yote ya filamu | Dola za US. 230,418,342 |
Space Jam ni filamu ya 1996 ya Kimarekani, ambayo imechanganya katuni-na-waigizaji wa kweli, yaani, watu. Ndani ya filamu hii anakuja Michael Jordan, Bugs Bunny (sauti yake imeigizwa na Billy West) na wahusika wengine wote wa Looney Tunes. Filamu ilitayarishwa na Ivan Reitman, na kuongozwa na Joe Pytka (upande wa live-action), Tony Cervone, na Bruce W. Smith (upande katuni). Filamu ilitolewa kwenye maukumbi na Warner Bros. Family Entertainment mnamo 15 Novemba 1996. Filamu inachezwa kivingine kwamba kwanini Michael amerudi tena kwenye mpira wa kikapu, mara hii ameshawishiwa na Bugs Bunny na wenzake.
Hadithi
[hariri | hariri chanzo]Akiwa kama nyota wa NBA Michael Jordan amestaafu kucheza mpira wa kikapu ili mradi kujiendeleza zaidi katika micheza baseball, Mister Swackhammer, mmiliki wa hifadhi ya nje ya dunia ya "Moron Mountain", anaomba vivutio vipya kwa ajili ya hifadhi yake inayoanguka. Anatuma watumishi wake, "Nerdlucks", kwenda kuwateka Looney Tunes, ambao wanaishi chini kabisa ya uso wa Dunia. Wakina Looney Tunes wakalipiza kisa kwa kushindana na Nerdlucks kwa mchezo wa mpira wa kikapu (wakionekana kama siyo warefu). Kwa kujianda na mchezo huo, wakina Nerdlucks wakarudi Duniani kuja kuiba vipaji vya kina Charles Barkley, Patrick Ewing, Muggsy Bogues, Larry Johnson na Shawn Bradley. Wakina Nerdlucks wakatumia vipaji walivyoiba kuwa "Mijitu ya Kutisha", viumbe virefu kabisa ambavyo wakina Looney Tunes hawana uwezo wa kushinda wao wenyewe. Kuwashinda wale, wakina Looney Tunes wakamwita Michael Jordan na msaidizi wake Stan Podolak. Baada ya punde, mchezo ukaanza kati ya wakina Looney Tunes na ile Mijitu, lakini wakina Looney Tunes wakaumizwa vibaya-vibaya na mtindo wa uchezaji wa fujo wa ile Mijitu, hivyo haiwezekani mpaka Jordan pekee, Bugs, Lola na Daffy wamebaki wakisimama na kuacha akicheza mtu mmoja tu. Bill Murray, huwa marafiki na mtayarishaji wa filamu, ana uwezo wa kuingia katika ulimwengu wa Looney Tunes na kujiunga na kikosi chao, akatwaa kizuizi. Kileleni mwa mchezo, wakina Tunes wakawa wapo chini kwa moja na juu ya Michael Jordan kushinda pointi ya mwisho kwa ajili ya timu yake. Kwa kutumia mkono wake usio-maarufu na -wenye kurefuka, Michael Jordan ameweza kufanikisha kuweka mpira kwenye kikapu na kushinda mchezo huo. Baada ya hapo, wakina Looney Tunes wakamrudisha Michael Jordan katika sayari yake ya Dunia, ambapo alirejesha kipaji kilichoibiwa kwa wamiliki halisi na kurejea kwelikweli kwenye NBA.
Washiriki
[hariri | hariri chanzo]- Michael Jordan kacheza kama jina lake.
- Brandon Hammond amecheza kama Michael Jordan akiwa kama na umri wa miaka kumi.
- Wayne Knight kama Stan Podolak.
- Billy West amechangia sauti ya:
- Bugs Bunny
- Elmer Fudd, ambaye alikuwa akitaka kifoc cha Bugs Bunny. Anachezea timu ya kina Looney Tunes.
- Dee Bradley Baker amecheza sauti ya:
- Daffy Duck.
- The Tasmanian Devil, mwehu na zee la mbwembwe anayechezea timu ya Looney Tunes.
- A bull
- Theresa Randle kacheza kama Juanita Jordan, mke wa Michael Jordan.
- Danny DeVito amecheza sauti ya Mister Swackhammer, kubwa la maadui la kwenye filamu. Yeye ndiye mmiliki wa hifadhi ya "Moron Mountain".
- Manner Washington kacheza kama Jeffrey Jordan, mtoto mkubwa wa Michael Jordan.
- Bob Bergen amecheza sauti ya:
- Hubie and Bertie, panya wiwili ambao wamecheza kama watangazaji wa mchezo huu.
- Marvin the Martian, kiumbe cha dunia nyingine kilicheza kama refa wa mchezo huu.
- Porky Pig, nguruwe mwenye kigugumizi anayeichezea timu ya kina Looney Tunes.
- Tweety, Kurumbiza wa Njano anayechezea timu ya Looney Tunes.
- Eric Gordon kacheza kama Marcus Jordan, mtoto mdogo wa Michael Jordan.
- Penny Bae Bridges kacheza kama Jasmine Jordan, binti wa Michael Jordan.
- Bill Farmer amechangia sauti ya:
- June Foray amechangia sauti ya Granny
- Kath Soucie amechangia sauti ya Lola Bunny, sungura wa kike anayeichezea timu ya Looney Tunes.
- Maurice LaMarche amechangia sauti ya Pepé Le Pew, kicheche mwenye lafudhi ya Kifaransa, anayeichezea timu ya Looney Tunes.
- Larry Bird amecheza kama jina lake akiwa kama rafiki wa Michael Jordan ambaye aliungana naye kwa ajili ya mchezo wa golf.
- Bill Murray amecheza kama jina lake
- Thom Barry kacheza kama James Jordan, baba wa Michael Jordan.
Charles Barkley, Patrick Ewing, Muggsy Bogues, Larry Johnson, Shawn Bradley, Ahmad Rashad, Del Harris, Vlade Divac, Cedric Ceballos, Jim Rome, Paul Westphal na Danny Ainge wameonekana kama majina yao kwenye filamu hii. Bebe Drake amecheza kama mfanya kazi wa ndani wa Michael Jordan. Sauti za kina Nerdlucks zilichezwa na Jocelyn Blue (Pound), Charity James (Blanko), June Melby (Bang), Catherine Reitman (Bupkus) na Colleen Wainwright (Nawt); sauti za ile Mijitu zilichezwa na Darnell Suttles (Pound), Steve Kehela (Blanko), Joey Camen (Bang), Dorian Harewood (Bupkus) and T.K. Carter (Nawt). Dan Castellaneta na Patricia Heaton ameuza sura akiwa kama kimwana wa Nerdlucks (kwa kusingizia) alikaa pembeni kabisa wakati wa mchezo wa mpira wa kikapu.
Vibwagizo
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti rasmi ya Space Jam
- Space Jam at the Internet Movie Database
- (Kiingereza) Space Jam katika Allmovie
- Space Jam at Box Office Mojo