Eric Gordon

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Eric Ambrose Gordon Jr. (amezaliwa Desemba 25, 1988)[1] ni mchezaji wa mpira wa kikapu kutokea nchi ya Marekani anachezea timu ya Los Angeles Clippers katika Chama cha mpira wa Kikapu Marekani (NBA). Akiwa shule ya sekondari, alipewa jina la "Mr. Basketball" wa Indiana wakati wa mwaka wake wa mwisho wa masomo alipokuwa akicheza katika Shule ya sekondari ya North Central. Kwa sehemu, anajulikana, kwa ushindani uliokuwepo wa kuajiriwa kwake kati ya Chuo Kikuu cha Illinois na Chuo Kikuu cha Indiana katika majira ya joto ya mwaka 2006; kwa sababu ya talanta ya Gordon na kiwango cha juu cha uchezaji wake mwaka huo, kuajiriwa kwake ilikuwa mada ya kutangazwa kwenye vyombo vya habari (media).

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Eric Gordon Stats, Height, Weight, Position, Draft Status and more (en). Basketball-Reference.com. Iliwekwa mnamo 2023-05-25.