Michael Jordan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Michael Jordan
Jordan Aprili 2014

Michael Jeffrey Jordan (pia anajulikana kwa jina lake la utani, MJ; alizaliwa 17 Februari 1963) ni mchezaji mstaafu wa mpira wa kikapu wa Marekani, mfanyabiashara, na mmiliki mkuu na mwenyekiti wa Hornet Charlotte wa Chama cha Mpira wa Kikapu Marekani (NBA).

Jordan alicheza misimu 15 katika NBA akiwa Chicago Bulls na Washington Wizards. Historia yake kwenye tovuti ya NBA inasema: "Kwa kulazimisha, Michael Jordan ni mchezaji mkubwa wa mpira wa kikapu kwa wakati wote".

Jordan alikuwa mmojawapo ya wanariadha wa soko la kizazi chake na alionekana kuwa muhimu katika kuendeleza NBA duniani kote katika miaka ya 1980 na miaka ya 1990.

Jordan alicheza mpira wa kikapu wa vyuoni kwa misimu mitatu chini ya kocha Dean Smith akiwa na North Carolina Tar Heels.Akiwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza alikuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Tar Heels ambayo ilichukuwa ubingwa mnamo 1982.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. NBA.com: Michael Jordan Bio. web.archive.org (2006-09-02). Jalada kutoka ya awali juu ya 2006-09-02. Iliwekwa mnamo 2023-05-18.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Michael Jordan kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.