Sophie Aberle
Sophie Bledsoe Aberle (21 Julai 1896 - Oktoba 1996) alikuwa mwanaanthropolojia, daktari na mtaalamu wa lishe wa Marekani aliyejulikana kwa kazi yake na watu wa Pueblo.
Alikuwa mmoja wa wanawake wawili walioteuliwa kwa mara ya kwanza kwenye Bodi ya Kitaifa ya Sayansi ya Marekani.[1]
Maisha ya awali na elimu
[hariri | hariri chanzo]Sophie Bledsoe Herrick alizaliwa mnamo 1896 akiwa mtoto wa Albert na Clara S. Herrick huko Schenectady, New York. Bibi yake mzazi na wajina wake alikuwa mwandishi Sophia Bledsoe Herrick. Sophie alipata elimu akiwa nyumbani na alifunga ndoa akiwa na umri wa miaka 21 na mwanamume aliyeitwa Aberle.[2][3] Alianza kuhudhuria Chuo Kikuu cha California huko Berkeley lakini akahamia Chuo Kikuu cha Stanford, na kupata shahada ya kwanza mnamo 1923,[3] stashahada ya uzamili mnamo 1925, na stashahada ya uzamivu katika jenetikia mnamo 1927. Kisha alienda shule ya matibabu, na kupata udaktari wa binadamu kutoka Chuo Kikuu cha Yale mnamo 1930. Akiwa mwanafunzi, alifanya kazi kama mwanahistoria msaidizi, mwanaeembriolojia, na daktari wa neva, na kama mwalimu wa anthropolojia.[4][5]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Collection: Sophie D. Aberle Papers | New Mexico Archives Online". nmarchives.unm.edu. Iliwekwa mnamo 2024-03-09.
- ↑ Ferris, Kathlene (2014-09-16). "Sophie D. Aberle and the United Pueblos Agency, 1935-1944". History ETDs.
- ↑ 3.0 3.1 "Aberle, Sophie D., 1899- - Social Networks and Archival Context". snaccooperative.org. Iliwekwa mnamo 2024-03-09.
- ↑ "Aberle, Sophie D., 1899- - Social Networks and Archival Context". snaccooperative.org. Iliwekwa mnamo 2024-03-09.
- ↑ Martha J. Bailey (1994). American women in science. Internet Archive. ABC-CLIO. ISBN 978-0-87436-740-9.
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sophie Aberle kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |