Slothi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Slothi
Slothi koo-kahawia mwenye vidole vitatu Bradypus variegatus
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele)
Nusungeli: Eutheria
Oda: Pilosa
Nusuoda: Folivora (Wanyama kama slothi)
Ngazi za chini

Familia 2:

Slothi (kutoka Kiing.: sloth) ni mamalia wa ukubwa wa kawaida wa familia Megalonychidae (slothi wenye vidole viwili) na Bradypodidae (slothi wenye vidole vitatu) wanaoainisha katika spishi sita. Wao ni wanachama wa oda Pilosa na kwa hivyo huwa uhusiano na armadilo na wala-sisimizi walio na kucha sawa na za slothi. Slothi wanaoishi sasa huishi mitini mwa misitu mizito ya Amerika ya Kati na Kusini, na hujulikana kwa kusonga polepole, kwa hivyo walipewa jina la slothi ambalo kwa Kiingereza lina maana ya "mvivu".

Taksonomia na majina[hariri | hariri chanzo]

Nusuoda ya kitaksonomia ya slothi ni Folivora, wakati mwingine anaitwa Phyllophaga. Majina mawili yamaanisha "mla-majani"; kutoka Kilatini na Kigiriki. Majina ya mnyama huyu yanayotumiwa na makabila ya Ekwado ni ritto, rit na ridette, ambayo humaanisha "kulala", "kula" na "mchafu" kutoka kabila ya Watagaeri wa Huaorani.

Ekolojia[hariri | hariri chanzo]

Slothi wanaainishwa kama wala-majani kwa sababu kwa kawaida hula maua na majani. Slothi wengine wenye vidole viwili hula wadudu, watambaazi wadogo na ndege. Majani wanayoyakula hayawatolei nishati nyingi, kwa hivyo, slothi wana matumbo makubwa. Slothi hawawezi kuishi nje ya misitu ya mvua ya kitropiki ya Amerika Kusini na ya Kati, katika mazingira hayo slothi ni viumbe wanaishi vizuri.

WikiLettreMini.svg Makala hii kuhusu "Slothi" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili sloth kutoka lugha ya Kiingereza. Neno (au maneno) la jaribio ni slothi.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.