Nenda kwa yaliyomo

Slothi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Folivora)
Slothi
Slothi koo-kahawia mwenye vidole vitatu Bradypus variegatus
Slothi koo-kahawia mwenye vidole vitatu
Bradypus variegatus
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele)
Nusungeli: Eutheria
Oda: Pilosa (Walasisimizi na slothi)
Nusuoda: Folivora (Slothi)
Delsuc et al., 2001
Ngazi za chini

Familia 2, jenasi 2, spishi 6:

Slothi (kutoka Kiing.: sloth) au wavivu-miti ni mamalia wa ukubwa wastani wa familia Choloepodidae (slothi wenye vidole viwili) na Bradypodidae (slothi wenye vidole vitatu) wanaoainishwa katika spishi sita. Ni wana wa oda Pilosa na kwa hivyo huwa uhusiano na armadilo na walasisimizi walio na kucha sawa na zile za slothi. Spishi zinazopo hadu sasa huishi mitini mwa misitu mizito ya Amerika ya Kati na ya Kusini, na hujulikana kwa kusonga polepole, kwa hivyo walipewa jina la slothi ambalo kwa Kiingereza lina maana ya "mvivu", au kwa Kiswahili mvivu-miti.

Taksonomia na majina

[hariri | hariri chanzo]

Nusuoda ya kitaksonomia ya slothi ni Folivora, wakati mwingine inaitwa Phyllophaga. Majina mawili yanamaanisha "mla-majani"; kutoka Kilatini na Kigiriki. Majina ya wanyama hawa yanayotumiwa na makabila ya Ekwado ni ritto, rit na ridette, ambayo humaanisha "kulala", "kula" na "mchafu" kutoka kabila ya Watagaeri wa Huaorani.

Ekolojia

[hariri | hariri chanzo]

Slothi wanaainishwa kama wala-majani kwa sababu hula maua na majani kwa kawaida. Slothi wengine wenye vidole viwili hula wadudu, watambaazi wadogo na ndege. Majani wanayoyakula hayawatolei nishati nyingi, kwa hivyo, slothi wana utumbo mkubwa. Slothi hawawezi kuishi nje ya misitu ya mvua ya kitropiki ya Amerika ya Kusini na ya Kati, katika mazingira hayo slothi ni viumbe wanaoishi vizuri.

Makala hii kuhusu "Slothi" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili sloth kutoka lugha ya Kiingereza. Neno (au maneno) la jaribio ni slothi.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.