Shambulio la mfululizo la kifafa
Status epilepticus | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Kundi Maalumu | Neurology, epileptology |
ICD-10 | G41. |
ICD-9 | 345.3 |
eMedicine | emerg/554 article/908394 |
MeSH | D013226 |
Shambulio la mfululizo la kifafa (kifupi: SMK; kwa Kilatini status epilepticus) ni tukutiko la kifafa la zaidi ya dakika tano au matukutiko zaidi ya moja katika muda wa dakika tano bila mtu kurudia hali ya kawaida. Matukutiko yanaweza kuwa ya misukosuko yaliyo na mtindo wa kubana na kunyosha mikono na miguu au ya aina ambazo hazihusishi ubanaji kama vile kifafa cha muda mfupi au nusu tukutiko changamani. Shambulio la mfululizo la kifafa ni hatari kwa uhai hasa iwapo matibabu yatacheleweshwa.[1]
Kisababishi na utambuzi
[hariri | hariri chanzo]Shambulio la mfululizo la kifafa linaweza kutokea kwa wale walio na historia ya kifafa na pia walio na tatizo la mfumo wa neva ya kati.[2] Matatizo hayo ya ubongo yanaweza kujumuisha jeraha, maambukizi au kupooza miongoni mwa mengine.[2] Utambuzi huhusisha kuchunguza sukari ya damu, kupiga picha ya kichwa, vipimo kadhaa vya damu, na elektroensefalogramu. Matukutiko ya kisaikojeni yasiyo ya kifafa yanaweza kutokea kwa njia sawa. Hali nyingine ambazo zinaweza kuonekana kuwa SMK hujumuisha: hipoglisimia, matatizo ya kutembea, meninjitisi, na deliriamu miongoni mwa mengine.[1]
Matibabu na utambuzi
[hariri | hariri chanzo]Benzodiazepini ndiyo dawa ya kwanza inayopendelewa ambapo baada yake fenintoini hutumika.[1] Benzodiazepini zinazopatikana ni sindano ya kudunga ndani ya mishipa lorazepamu, na pia sindano ya misuli ya midazolamu.[3]
Baadhi ya dawa nyingine zinazoweza kutumiwa iwapo hizi hazifai ni kama vile asidi ya valproiki, fenobabitali, propofoli au ketamini. Intubesheni inaweza kuhitajika ili kudumisha njia ya hewa.
Tiba ya kutumia chakula kama Ketojeniki, tena bangi hutumiwa pia. Serikali ya Marekani ni nchi ya kwanza duniani kutoa kibali kwa kampuni iliyotengeneza tiba ya kifafa kwa kutumia bangi.
Kisababishi, umri wa mtu, na muda ambao tukutiko hudumu ni vipengele muhimu katika matokeo.[2] Shambulio la mfululizo la kifafa hutokea katika hadi watu 40 kati ya watu 100,000 kila mwaka.[2] Hufikisha hadi asilimia 1 ya watu ambao hutembelea kitengo cha dharura.[1] Kati ya asilimia 10 hadi 30 ya watu walio na shambulio la mfululizo la kifafa hufariki katika muda wa siku 30.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 Al-Mufti, F; Claassen, J (Okt 2014). "Neurocritical Care: Status Epilepticus Review". Critical Care Clinics. 30 (4): 751–764. doi:10.1016/j.ccc.2014.06.006. PMID 25257739.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 Trinka, E; Höfler, J; Zerbs, A (Septemba 2012). "Causes of status epilepticus". Epilepsia. 53 Suppl 4: 127–38. doi:10.1111/j.1528-1167.2012.03622.x. PMID 22946730.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Prasad, M; Krishnan, PR; Sequeira, R; Al-Roomi, K (Sep 10, 2014). "Anticonvulsant therapy for status epilepticus". The Cochrane database of systematic reviews. 9: CD003723. PMID 25207925.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Habari kuhusu kifafa toka shirika lisilo la kiserikali la Uingereza Matthew's Friends.
- Shambulio la mfululizo la kifafa katika Open Directory Project
- Habari kuhusu kifafa toka The Charlie Foundation.
- epilepsy.com: Tiba za kifafa kwa kutumia chakula kama Ketojeniki. Archived 25 Desemba 2013 at the Wayback Machine.
- Mahojiano kuhusu Mlo wa Ketojeniki.
- Jinsi Mlo wa Ketojeniki unavyofanya kazi.
- Mwongozo kuhusu Mlo wa Ketojeniki Archived 13 Septemba 2017 at the Wayback Machine..
- Tiba ya kifafa kwa kutumia bangi.
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Shambulio la mfululizo la kifafa kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |