Nenda kwa yaliyomo

Serati

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Serati
Nchi Ufaransa
Kazi yake askofu

Serati (pia: Cerat, Ciratus, Ceretius, Ceratus, Ceras, Gerase; alifariki 450 hivi) alikuwa askofu wa Grenoble katika Burgundy, leo nchini Ufaransa, kwa miaka kumi, akidumisha imani sahihi kati ya waumini wake dhidi ya Uario wa wavamizi wa nchi ile.

Kutokana na msimamo huo, alimshukuru Papa Leo I kwa barua aliyomtumia Patriarki Flaviani wa Konstantinopoli.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Heshima hiyo ilithibitishwa na Papa Pius X tarehe 9 Desemba 1903.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 6 Juni.[1]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.