Senorina

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Senorina.

Senorina (kwa Kireno: Senhorinha; Vieira do Minho, 942 hivi - Basto, 22 Aprili 982) alikuwa bikira nchini Ureno, mwenye undugu na Rudesindo[1].

Kisha kuingia katika monasteri ya Wabenedikto huko Vieira, iliyoongozwa na Godinha, dada wa mzazi wake, alimrithi kama abesi[1][2] halafu akahamishia monasteri huko Basto, karibu na Braga[2] . Jumuia ilipokosa chakula, alimuomba Mungu, naye akawapatia mara [3][4].

Alitangazwa mtakatifu na askofu Paio Mendes wa Braga mwaka 1130[5].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 22 Aprili[6].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 Online, Catholic. St. Senorina - Saints & Angels (en).
  2. 2.0 2.1 (1905) A dictionary of saintly women. London: George Bell & Sons / Internet Archive, 219-220. 
  3. https://www.santodelgiorno.it/santa-senorina-di-vieira/
  4. http://www.santiebeati.it/dettaglio/50360
  5. Santa Senhorinha de Basto: Canonização (pt). Igreja Paroquial de Santa Senhorinha de Basto (2018).
  6. Martyrologium Romanum
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.