Selerino wa Karthago

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Selerino wa Karthago (alifariki 251) alikuwa Mkristo wa mji huo (karibu na Tunisi ya leo) katika karne ya 3.

Kama bibi yake Selerina, na Laurenti na Ignasi, askari ndugu wa wazazi wake, alikubali kufungwa pingu na kuteswa kwa namna mbalimbali na hatimaye kuuawa kwa ajili ya imani yake.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa hasa tarehe 3 Februari[1][2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.