Nenda kwa yaliyomo

Selerina wa Karthago

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Selerina wa Karthago (alifariki 250 hivi) alikuwa mwanamke Mkristo wa mji huo (karibu na Tunisi ya leo) katika karne ya 3.

Alikubali kufungwa pingu na kuteswa kwa namna mbalimbali na hatimaye kuuawa kwa ajili ya imani yake katika dhuluma ya kaisari Decius.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa hasa tarehe 3 Februari[1] pamoja na Laurenti na Ignasi[2].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.