Nenda kwa yaliyomo

Khamis Said Gulamali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Seif Khamis Said Gulamali)

Seif Khamis Said Gulamali (amezaliwa 3 Oktoba 1984) ni mwanasiasa wa Tanzania na mwanachama wa Chama cha kisiasa cha Chama cha Mapinduzi (CCM). Amechaguliwa kuwa mbunge wa Manonga kwa miaka 20152020. [1]

Amezaliwa katika jiji la Mwanza. Amesoma shule mbili tofauti za msingi: alisoma katika Shule ya Msingi Kharumwa Wilaya ya Nyang'hwale (sasa Mkoa wa Geita) kwa kuanzia darasa la 1 mpaka darasa la 3 na kuhamia Tabora ambako alisoma katika Shule ya Msingi Chemchem.

Sekondari pia amesoma katika shule mbili: alianzia Shule ya Sekondari Kazima Sekondari Kidato cha Kwanza mwaka 2001 na baadae alihamia Shule ya Sekondari Mihayo (St'Mary's) kwa kuendelea na Kidato cha Pili mpaka Kidato cha Nne mwaka 2002-2004.

Alijiunga na Shule ya Sekondari Jamhuri ya Dodoma kwa Kidato cha 5 na 6 mwaka 2006-2008 na kujiunga na Chuo ambapo aliweza kusomea Masuala ya Usafirishaji katika Chuo Cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa Shahada ya Freight Clearing and Forwading kuanzia mwaka 2008 mpaka 2011.

  1. Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017