Saturus wa Karthago
Saturus wa Karthago ni mmoja wa mashahidi wa imani ya Kikristo waliouawa tarehe 7 Machi 203 mjini Karthago wakati wa dhuluma dhidi ya Wakristo chini ya serikali ya Kaisari Septimius Severus (193-211).
Anaheshimiwa tangu kale kati ya watakatifu wafiadini pamoja na watakatifu Perpetua na Felista wanaojulikana zaidi kama mashahidi Wakristo wa Afrika ya Kaskazini.
Pamoja na akina mama hao vijana na wanaume wengine 3 walikamatwa pamoja na kutupwa jela. Jinsi ilivyokuwa kawaida walipewa nafasi ya kuachana na Ukristo lakini wote walisimama imara wakabatiwza gerezani.
Walihukumiwa adhabu ya kifo katika uwanja wa michezo mbele ya watu wengi. Hukumu ilitekelezwa kwa njia ya wanyamapori. Waliraruliwa na wanyama mbalimbali, wakamalizwa kwa upanga, isipokuwa Sekondinus aliyefariki gerezani.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe ya kifodini chao[1].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |