Perpetua Mtakatifu



Perpetua (181 - 7 Machi 203) alikuwa mama kijana mjini Karthago (leo nchini Tunisia) wakati wa Dola la Roma alipouawa kama shahidi wa imani ya Kikristo.
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi, Waanglikana, Walutheri na wengineo kati ya watakatifu wafiadini na sikukuu yake ni tarehe 7 Machi[1].
Perpetua anakumbukwa pamoja na mtumwa na rafiki yake Felista na wavulana wanne ambao aliuawa pamoja nao: Saturus, Revokatus, Saturninus na Sekondinus.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Perpetua alikuwa binti wa familia tajiri.
Kwenye umri wa miaka 21 aliolewa akapata mtoto. Wakati ule alijiandaa kubatizwa pamoja na watumwa wake Felista na Revocatus na kijana mwingine aliyeitwa Saturninus. Walikamatwa pamoja na mwalimu wao Saturus na wakatekumeni wengine wa kike katika wimbi la dhuluma dhidi ya Wakristo chini ya serikali ya Kaisari Septimius Severus (193-211).
Kwanza Perpetua alifungwa ndani na kupewa nafasi ya kuachana na imani yake. Alipokataa alihukumiwa adhabu ya kifo pamoja na wenzake. Gerezani walipokea ubatizo.
Perpetua alibembelezwa sana na babaye Mpagani aachane na Ukristo na kuokoa uhai wake, lakini alikataa.
Pamoja na wenzake aliuawa katika uwanja wa michezo mbele ya watu wengi. Hukumu ilitekelezwa kwa njia ya wanyamapori. Yeye na Felista walitokea gerezani kuingia uwanjani wakiwa wafurahivu kama kwenda mbinguni [2].
Heshima baada ya kifo
[hariri | hariri chanzo]Heshima iliyotolewa mara kwa wafiadini hao ilienea haraka katika Kanisa lote.
Masalia ya Perpetua yalihamishwa mara kadhaa kutoka na matatizo ya kihistoria. Hatimaye yamehifadhiwa huko Vierzon (Ufaransa).
Matendo ya Perpetua na Felista
[hariri | hariri chanzo]"Matendo ya Perpetua na Felista"[3] ni maandishi ya pekee kwa sababu kuna kumbukumbu ambazo zinasimulia habari zake gerezani na wataalamu huamini ya kwamba zimeandikwa na Perpetua mwenyewe (sura III-X). Kama hii ni kweli, ni maandiko ya kale kabisa ya mwanamke Mkristo katika historia iliyotunzwa.
Filamu
[hariri | hariri chanzo]- Perpetua: Early Church Martyr (2009) - documentary.
- Torchlighters: The Perpetua Story (2009) - animated DVD for children ages 8–12.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Mabradha wa Shule za Kikristo
- Orodha ya Watakatifu Waaugustino
- Orodha ya Watakatifu Wabazili
- Orodha ya Watakatifu Wabenedikto
- Orodha ya Watakatifu Wadominiko
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
- Orodha ya Watakatifu Wajesuiti
- Orodha ya Watakatifu Wakarmeli
- Orodha ya Watakatifu Wakolumbani
- Orodha ya Watakatifu Wamersedari
- Orodha ya Watakatifu Waoratori
- Orodha ya Watakatifu Wapasionisti
- Orodha ya Watakatifu Wapremontree
- Orodha ya Watakatifu Waredentori
- Orodha ya Watakatifu Wasalesiani
- Orodha ya Watakatifu Waskolopi
- Orodha ya Watakatifu Wateatini
- Orodha ya Watakatifu Watrinitari
- Orodha ya Watakatifu Watumishi wa Maria
- Orodha ya Watakatifu Wavinsenti
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/22950
- ↑ Sehemu imetafsiriwa kwa Kiswahili katika Masomo ya Breviari - Sikukuu za Bwana, za Bikira Maria na za Watakatifu - Ndanda Mission Press 1978, uk 81-83.
Marejeo ya Kiswahili
[hariri | hariri chanzo]- John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 82-84
- Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 67-68
- Maurice Soseleje, Kalendari yetu – Maisha ya Watakatifu – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Peramiho 1986 – ISBN 9976-63-112-X, uk. 26
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Matendo ya Mt. Perpetua kwa Kilatini, Kigiriki na Kiingereza. Kitabu chote katika www.earlychurchtexts.com.
- "Matendo ya Perpetua na Felista" katika tafsiri ya Kiingereza.
- Medieval Sourcebook: The Passion of Saints Perpetua and Felicity. Ilihifadhiwa 6 Machi 2011 kwenye Wayback Machine. From W.H. Shewring, trans. The Passion of Perpetua and Felicity, (London: 1931), modernized.
- Henry Wace, A Dictionary of Christian Biography and Literature to the End of the Sixth Century A.D. 1911
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |