Nenda kwa yaliyomo

Felista Mtakatifu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kifodini cha Mt. Perpetua, Felista na wenzake katika vioo vya kanisa la Bikira Maria huko Vierzon (karne ya XIX).

Felista (kutoka Kilatini "Felicitas" - Heri ) ni mmoja wa mashahidi wa imani ya Kikristo waliouawa tarehe 7 Machi 203 mjini Karthago wakati wa dhuluma dhidi ya Wakristo chini ya serikali ya Kaisari Septimius Severus (193-211).

Anaheshimiwa kati ya watakatifu wafiadini wanaojulikana zaidi kama mashahidi Wakristo wa Afrika ya Kaskazini.

Mama huyo kijana anakumbukwa pamoja na rafiki yake mtakatifu Perpetua na wengine 4 wanaume tarehe ya kifodini chao[1].

Felista alikuwa kati ya watumwa wa familia ya Perpetua sawa na Revocatus. Pamoja nao na Saturninus alikuwa mmoja wa wanafunzi wa imani ya kikristo mjini Karthago waliojiandaa kubatizwa. Kundi lote likakamatwa pamoja na kutupwa jela. Jinsi ilivyokuwa kawaida walipewa nafasi ya kuachana na Ukristo lakini wote walisimama imara wakabatizwa gerezani. Walihukumiwa adhabu ya kifo katika uwanja wa michezo mbele ya watu wengi. Hukumu ilitekelezwa kwa njia ya wanyamapori. Felista alikuwa mjamzito mwenye uchungu wa kujifungua, hivyo kisheria angestahili kuachiliwa, kumbe alionekana mtulivu mbele ya wanyama hao [2].

Matendo ya Perpetua na Felista

[hariri | hariri chanzo]

"Matendo ya Perpetua na Felista"[3] ni maandishi ya pekee kwa sababu kuna kumbukumbu ambazo zinasimulia habari zake gerezani na wataalamu huamini ya kwamba zimeandikwa na Perpetua mwenyewe (sura III-X). Kama hii ni kweli, ni maandiko ya kale kabisa ya mwanamke Mkristo katika historia iliyotunzwa.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Martyrologium Romanum
  2. https://www.santiebeati.it/dettaglio/22950
  3. Sehemu imetafsiriwa kwa Kiswahili katika Masomo ya Breviari - Sikukuu za Bwana, za Bikira Maria na za Watakatifu - Ndanda Mission Press 1978, uk 81-83.
  • Perpetua: Early Church Martyr (2009) - documentary.
  • Torchlighters: The Perpetua Story (2009) - animated DVD for children ages 8–12.

Marejeo ya Kiswahili

[hariri | hariri chanzo]
  • John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 82-84
  • Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 68
  • Maurice Soseleje, Kalendari yetu – Maisha ya Watakatifu – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Peramiho 1986 – ISBN 9976-63-112-X, uk. 26

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.