Uwanja wa michezo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uwanja wa Olimpiki huko Ugiriki
Uwanja wa Messene ulio na ngazi za kuketi kwa mawe na nafasi za kusimama zisizoimarishwa
Koloseo huko Roma. Uwanja huu wa michezo ni mfano wa viwanja vya kisasa
Uwanja wa michezo wa Strahov huko Praha (nchini Ucheki), ni uwanja mkubwa zaidi wa nyakati za kisasa

Uwanja wa michezo (Kilat. + Kiing. stadium) ni mahali pa mashindano ya michezo. Mara nyingi umezungukwa na majengo ambayo yanaweza kufunguliwa juu na kuwezesha umma kutazama onyesho hilo kwa kutumia nafasi za kusimama au kukaa. Viwanja mara nyingi hutumiwa pia kwa matamasha na mikutano ya hadhara.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Viwanja vya michezo vilipatikana tayari katika miji mingi ya Ugiriki ya Kale ambako mashindano yalitekelezwa kwa heshima ya miungu. Mashuhuri hasa vilikuwa viwanja vya Olimpia na Delfi[1].

Katika Roma ya Kale viwanja vilitumiwa hasa kwa matamasha ya mapigano na uwindaji. Mfano mashuhuri ni Koloseo wa Roma. Jengo hili lilikuwa kielelezo wa viwanja vingi vya kisasa.

"Uwanja wa Busch" (baseball) huko St. Louis, Missouri (Marekani)

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. World Stadiums - Architecture :: Stadium history. www.worldstadiums.com. Jalada kutoka ya awali juu ya 2021-10-05. Iliwekwa mnamo 2021-06-09.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.