Sao Tome (kisiwa)
Mandhari
Sao Tome (kwa Kireno São Tomé) ni kisiwa cha bahari ya Atlantiki karibu na pwani ya Afrika Magharibi.
Kimeundwa na kilele cha mlima wa safu za volkeno zilizokua kuanzia sakafu ya bahari hadi kufikia usoni pake. Volkeno hizi ni zimwe, si hai tena.
Ndicho kisiwa kikubwa cha Jamhuri ya Sao Tome na Principe, chenye takriban asilimia 90 za watu wote wa nchi.
Kisiwa hicho kina urefu wa rasi km 48 na upana wa km 32.
Kimo cha milima yake hufikia mita 2,024 juu ya UB.
Sao Tome iko kaskazini kidogo kwa mstari wa ikweta.
Jina la Sao Tome lamaanisha "Mtakatifu Thomas" kwa sababu Wareno walifika huko mara ya kwanza siku ya Mt. Thomas katika kalenda ya Kanisa Katoliki.
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Sao Tome (kisiwa) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |