Nenda kwa yaliyomo

Sanaa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sehemu ya La Gioconda, mchoro wa Leonardo da Vinci unaotunzwa huko Paris (Ufaransa).

Sanaa (kutoka neno la Kiarabu) ni ufundi anaoutumia mwanadamu ili kuwasilisha fikira au mawazo yaliyo ndani ya akili yake.

Vilevile sanaa ni uzuri unaojiibua katika umbo lililosanifiwa.

Kusanifu ni kuumba, kufanya jambo au kitu kwa kutumia ufundi/ustadi ili kiweze kuvutia watu kwa uzuri wake. Mtu hueleza hisia zinazomgusa kwa kutumia umbo fulani ambalo limesanifiwa.

Hivyo kazi yoyote ya sanaa inategemewa ioneshe ufundi wa hali ya juu ili iwe na mvuto kwa hadhira yake.

Tunaweza kuona kazi ya sanaa kupitia tanzu za fasihi, uchoraji, ususi, ufumaji, utarizi, uchongaji, ufinyanzi na kadhalika.

Kila umbo huwa na nyenzo zinazotumika katika kuliumba umbo hilo. Kwa mfano katika uchongaji kuna mti (gogo), panga, tezo, msasa, rangi na kadhalika.

Aina za sanaa

[hariri | hariri chanzo]

Sanaa za maonyesho

[hariri | hariri chanzo]
Sanaa ya uchoraji

Hizi ni sanaa ambazo uzuri wake hujitokeza katika umbo la kudumu, umbo ambalo linaweza kuhifadhiwa, hivi kwamba uzuri wake ukaendelea kuonekana wakati wowote ule.

Hizi ni baadhi tu ya aina za sanaa ambazo hutoa umbo la kudumu:

Sanaa za vitendo

[hariri | hariri chanzo]

Uzuri wa sanaa hizi umo katika umbo la vitendo, hivyo ilimradi kuupata uzuri huo ni lazima kutazama vitendo vinavyofanyika. Katika sanaa hizi lazima kuwe na chenye sifa kuu nne, ambazo ni:

  • Dhana ya kutendeka (tendo)
  • Mtendaji (fanani)
  • Uwanja wa kutendea
  • Watazamaji (hadhira)

Upekee wa fasihi

[hariri | hariri chanzo]

Kati ya hizo, fasihi ni tanzu ya pekee kwa sababu zifuatazo:

  1. Hutumia lugha.
  2. Huwa na wahusika maalumu.
  3. Huwa na muundo unaoeleweka.
  4. Hutumia mandhari halisi au ya kubuniwa.
  5. Huwa na mtindo unaoeleweka.
  6. Huwa na fani na maudhui.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
      . OCLC 237794267
      . http://www.econlib.org/library/Enc/Arts.html.
A look at how general economic principles govern the arts.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sanaa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.