Nenda kwa yaliyomo

Salawe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Salawe ni kata ya Wilaya ya Shinyanga Vijijini katika Mkoa wa Shinyanga, Tanzania yenye msimbo wa posta 37214. Kata ya Salawe inapakana na Mkoa wa Mwanza.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 25,010 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 17,247 waishio humo.[2]

Shughuli za kilimo

[hariri | hariri chanzo]

Shughuli kuu wanzofanya katika kata hii ni kilimo, na mazao makuu ambayo wanayategemea ni mpunga na mahindi mbali ya nyanya, viazi vitamu na ndengu pamoja na mboga za majani kama vile msusa. Mboga hizo za majani hupatikana kwa njia ya umwagiliaji.

Wakazi wa kata ya Salawe wanajishughulisha na kilimo cha jembe la mkono. Wakati wa uvunaji wa mazao jamii hujumuika kwa pamoja na mara nyingi mwenye mazao huandaa chakula kwa ajili ya shughuli hiyo.

Shughuli za biashara

[hariri | hariri chanzo]

Katika kata ya Salawe biashara inayoshika kasi kwa kiasi kikubwa ni biashara ya nyanya ambapo wakazi wengi hujishughulisha na zao hilo katika kuwaingizia kipato cha kila siku. Shughuli nyingine ni biashara za wanyama kama vile ng'ombe, kondoo, mbuzi pamoja na ndege kama vile kuku pamoja na biashara nyingine wanazofanya wanadamu.

Shughuli za kijamii

[hariri | hariri chanzo]

Katika shughuli za kijamii, kinapotokea kitu katika kata hii kama vile msiba watu wote hujumuika kwa pamoja.

Kuhusu ndoa, mwanamume hutoa mahari kubwa kama vile ng'ombe ishirini hususani mwanamke anapokuwa mweupe; ndoa nyingi hufanyika kipindi cha kilimo ambapo watu huweza kuwa na chakula cha kutosha kwa ajili ya tukio la harusi. Mahari hutolewa mara nyingi na baba wa mtoto anayeoa hususani mtoto wa kiume. Mara nyingi

Kata za Wilaya ya Shinyanga vjijini - Mkoa wa Shinyanga - Tanzania

Bukene | Didia | Ilola | Imesela | Iselamagazi | Itwangi | Lyabukande | Lyabusalu | Lyamidati | Masengwa | Mwakitolyo | Mwalukwa | Mwamala | Mwantini | Mwenge | Nsalala | Nyamalogo | Nyida | Pandagichiza | Puni | Salawe | Samuye | Solwa | Tinde | Usanda | Usule


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Shinyanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Salawe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.