Tinde

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Tinde ni kata ya Wilaya ya Shinyanga Vijijini katika Mkoa wa Shinyanga, Tanzania yenye msimbo wa posta 37210[1].

Kata ya Tinde ina vijiji vifuatavyo: Jomu, Nyambui, Kituli, Ngokolo, Buchama na Nhumbili.

Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 14,978 waishio humo.[2]

Kwa mujibu wa kitabu cha makadirio ya watu kilichotolewa na bunge mwaka 2016 idadi ya watu imeongezeka na kuwa 18,264.

Wakazi wengi wa Tinde ni wakulima, wakifuatiwa na wafanyakazi na wafanyabiashara.

Mazao yanayolimwa kwa wingi katika kata ya Tinde ni mahindi na mpunga. Mpunga ndio zao tegemezi ambalo linalimwa kwa wingi kwa ajili ya biashara na chakula vilevile.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Shinyanga vjijini - Mkoa wa Shinyanga - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Bukene | Didia | Ilola | Imesela | Iselamagazi | Itwangi | Lyabuke | Lyabusalu | Lyamidati | Masengwa | Mwakitolyo | Mwalukwa | Mwamala | Mwantini | Mwenge | Nsalala | Nyamalogo | Nyida | Pandagichiza | Puni | Salawe | Samuye | Solwa | Tinde | Usanda | Usule


Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Shinyanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tinde kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.