Nenda kwa yaliyomo

Rita Paulsen

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ritha Paulsen)
Rita Paulsen
Amezaliwa
Karagwe, Kagera,

Bendera ya Tanzania Tanzania

Kazi yake Mkurugenzi wa Bongo Star Search(BSS)


Rita Paulsen (anafahamika pia kama Madam Rita; alizaliwa wilaya ya Karagwe, Mkoa wa Kagera, 26 Februari 1977[1]) ni mjasiriamali, mhisani na mwanzilishi na mmiliki wa shirika linaloitwa Benchmark Productions.

Kwa sasa anaendesha kipindi chake katika televisheni kiitwacho Rita Paulsen Show.

Pia ni kati ya watu wa kwanza kuanzisha kampuni ya urembo na kuuchukulia urembo kama biashara[2].

Mnamo mwaka 2007 alianzisha shindano la uimbaji lijulikanalo kama Bongo Star Search (BSS), mradi ambao umejikita katika kuibua vipaji vya uimbaji kwa vijana mbalimbali nchini Tanzania. Kwa kufundisha taaluma za uimbaji kupitia hilo shindano la uimbaji. Mradi huu umewaibua wasanii wengi.Dhamira ni kuinua tasnia ya mziki ili kuwezesha kuinua vipaji vya vijana kupitia mziki.[3][4][5][6]

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Baba yake mzazi alikuwa na asili ya Ujerumani lakini alifariki Rita akiwa na umri mdogo.

Alipata elimu nchini Uganda na Zimbambwe. [7]

Ndoto zake zilikuwa awe mwanasheria ila mambo hayakuenda vizuri baada ya kupata ujauzito akiwa na umri wa miaka 14 [8].

Jamii yake haikumpokea vizuri. Hilo halikumfanya akate tamaa, hivyo alijitahidi kujikomboa katika maisha yake.[9]

Baadaye akaja kuwa mashuhuri na kutumia maisha yake ya nyuma kama kielelezo cha kuwafariji na kuwatia moyo mabinti wanaokumbana na matatizo ya mimba za utotoni[10].

Paulsen ni mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya utayarishaji wa vipindi vya televisheni, Benchmark Productions. Kampuni hiyo inazalisha kipindi cha televisheni cha Bongo Star Search, ambacho Paulsen ni jaji mkuu. Alianzisha kipindi hicho, Paulsen alihamasishwa na kipindi cha Kimarekani kilichojulikana kama American Idol. [9] Kama ilivyo kwa toleo la awali la kipindi icho cha Marekani, ni kugundua na kukuza vipaji vya kuimba, hasa vijana. [9] Kaulimbiu ya Bongo Star Search ni kuwasaidia vijana wa Kitanzania wenye vipaji vya muziki kuwa na ujuzi sahihi wa kuimba kupitia mashindano ya uimbaji. [11] [12] [13] [14]

Pia ni mtangazaji wa kipindi cha televisheni cha dakika 45 kinachoitwa, Rita Paulsen Show . Kipindi hiki kina sehemu tatu: 'Kubadilishana mawazo ya Maisha', 'Kona ya Mtu Mashuhuri' na 'Make Over'. [15] [16]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
  1. http://sanaa-central.spla.pro/en/file.person.rita-paulsen-madam-rita.40873.html
  2. http://sanaa-central.spla.pro/en/file.person.rita-paulsen-madam-rita.40873.html
  3. http://www.tanzaniatoday.co.tz/news/mshindi-wa-bongo-star-search-na-jinsi-fainali-hiyo-ilivyokuwa
  4. https://www.youtube.com/watch?v=uWjmHFc9f-s Millard Ayo 13 October 2015
  5. https://www.youtube.com/watch?v=mUzto8XHmuA
  6. https://www.youtube.com/watch?v=1eFkIm-EC1g
  7. "SPLA | Rita Paulsen (Madam Rita)". Spla (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-08-22.
  8. http://www.tanzaniatoday.co.tz/news/madam-rita-afunguka-nilizaa-katika-umri-mdogo-sana
  9. 9.0 9.1 9.2 Kubegeya, Maimuna (2015-06-21). "Kuzaa katika umri mdogo hakukunifanya nikate tamaa - Makala". Mwananchi. Iliwekwa mnamo 2018-05-04. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; name "mwananchi.co.tz" defined multiple times with different content
  10. http://www.tanzaniatoday.co.tz/news/madam-rita-afunguka-nilizaa-katika-umri-mdogo-sana
  11. "Tanzaniatoday.co.tz".
  12. https://www.youtube.com/watch?v=uWjmHFc9f-s Millard Ayo 13 October 2015
  13. Archived at Ghostarchive and the Wayback Machine: Bongo Star Search 2015 Dar Es Salaam Part 1. https://www.youtube.com/watch?v=mUzto8XHmuA.
  14. Archived at Ghostarchive and the Wayback Machine: Bongo Star Search 2015 Arusha Audition. https://www.youtube.com/watch?v=1eFkIm-EC1g.
  15. "The rise and rise of Rita Paulsen". 17 Juni 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-10-29.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  16. "Rita Paulsen Show S01E01 - - vimore.org". vimore.org.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rita Paulsen kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.