Rita Paulsen

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search


Rita Paulsen (anafahamika kwa jina lingine kama Madam Rita) ni mjasiriamali, mhisani na mwanzilishi na mmiliki wa kampuni iliyoitwa Benchmark Productions.

Kwa sasa anaendesha kipindi chake katika televisheni kiitwacho Rita Paulsen Show.

Pia ni kati ya watu wa kwanza kuanzisha kampuni ya urembo na kuuchukulia urembo kama biashara[1].

Mnamo mwaka 2007 alianzisha shindano la uimbaji lijulikalao kama Bongo Star Search (BSS), mradi ambao umejikita katika kuibua vipaji vya uimbaji kwa vijana mbalimbali nchini Tanzania kwa kufundisha taaluma za uimbaji kupitia hilo shindano la uimbaji. Mradi huu umewaibua wasanii wengi.

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Rita alizaliwa wilaya ya Karagwe, Mkoa wa Kagera, Tanzania[2] baba yake mzazi alikuwa na asili ya Ujerumani lakini alifariki Rita akiwa na umri mdogo.

Alipata elimu nchini Uganda na Zimbambwe. Ndoto zake zilikuwa awe mwanasheria ila mambo hayakuenda vizuri baada ya kupata ujauzito akiwa na umri wa miaka 14. Jamii yake haikumpokea vizuri. Hilo halikumfanya akate tamaa, hivyo alijitahidi kujikomboa katika maisha yake.[3]

Baadae akaja kuwa mashuhuri na kutumia maisha yake ya nyuma kama kielelezo cha kuwafariji na kuwatia moyo mabinti wanaokumbana na matatizo ya mimba za utotoni[4].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]