Richard Limo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rekodi za medali

Richard Limo (Kushoto) katika Amsterdam Marathon mwaka wa 2007
Men’s Wanariadha
Anawakilisha nchi Bendera ya Kenya Kenya
World Championships
Dhahabu 2001 Edmonton 5,000 m

Richard Kipkemei Limo (alizaliwa mnamo 18 Novemba 1980) mwanariadha kutoka taifa la Kenya. Yeye ni mtaalamu katika matukio ya masafa marefu. Alishinda medali ya dhahabu katika mita 5000 katika mchuano wa dunia katika riadha mwaka wa 2001.

Alizaliwa mwaka wa 1980 katika kijiji cha Cheptigit, wilayani Uasin Gishu. Baada ya shule ya msingi alihudhuria Polytechnic na kupokea daraja katika masomo ya waya na umeme mwaka wa 1996. Hakuwa ameanza kukimbia hadi mwaka wa 1997 wakati alijiunga na kambi ya mafunzo iliyoko karibu na nyumbani kwake. Mwaka uliyofuata alishinda medali ya fedha katika mbio ya vijana katika mchuano wa World Cross Country. Mwaka huo huo alivunja rekodi ya dunia ya vijana katika[mita 3000 kwa kukimbia kwa muda wa dakika 7:36.76, lakini alikosa mchuano wa dunia wa vijana. Mwaka wa 2001 akawa bingwa wa dunia na pia akawa mtendaji bora duniani wa mwaka huo ambao ulikuwa mwaka wa 2001 katika mbio za mita 5000 na muda wake wa dakika 12:56.72, bado ni rekodi yake bora ya kibinafsi. Tangu mwaka wa 2004 hajakuwa akionekana sana na vyombo vya habari, lakini tangu wakati huo amebadilika na kuanza kukimbia mbio ya masafa marefu zaidi ya marathon. Alichukua nafasi ya pili mwaka wa 2007 katika Amsterdam Marathon, mbio yake ya marathon ya kwanza ambapo rekodi yake bora na mpya ya kibinafsi (masaa 2:06:45)

Alimwoa kipenzi chake cha moyo Rose Tarus na wana watoto wawili, ambao walizaliwa miaka 2000 na 2002. Ana urefu wa mita 1.67 na uzito wa kilogramu 52. Hana uhusiamo wowote na Benjamin Limo au Felix Limo, ambao ni wanariadha wa nchi ya Kenya.

Majalio[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Mchuano Ukumbi Nafasi Ziada
1998 Mashindano ya dunia ya Cross Country Marrakech, Moroko 2 Junior
Michezo ya Jumuiya ya Madola Kuala Lumpur, Malaysia 3 mita 5000
Mashindano ya Kiafrika Dakar, Senegal 2 mita 3000
1999 Mashindano ya dunia ya Cross Country Belfast, Ireland ya Kaskazini 2 Ya vijana
Michezo ya All-Africa Johannesburg, Afrika Kusini 6 mita 5000
2000 Michezo ya Olimpiki Sydney, Australia 10 mita 5000
2001 Mashindano ya dunia ya Cross Country Oostende, Ubelgiji 32 Ya umbali
Mchuano wa dunia Edmonton, Kanada 1 mita 5000
Fainali ya IAAF Grand Prix Melbourne, Australia 5 mita 5000
2002 Mashindano ya dunia ya Cross Country Dublin, Ireland 4 Ya urefu
IAAF Grand Prix Final Paris, Ufaransa 7 mita 5000
mwaka wa(2003). Mashindano ya dunia ya Cross Country Lausanne, Uswisi 4 Ya urefu
IAAF World Athletics Final Monako 2 mita 5000
2004 Mashindano ya dunia ya Cross Country Brussels, Ubelgiji 32 Ya urefu

Mbio za marathon[hariri | hariri chanzo]

  • 2007 Amsterdam Marathon - 2 (AS 2:06:45)
  • 2008 Rotterdam Marathon - 4
  • 2008 Chicago Marathon] - 10
  • 2009 Rotterdam Marathon - 9 [1]

Ubora wa kibinafsi[hariri | hariri chanzo]

  • Mita 1500 - dakika 3:37.59 (1999)
  • Mita 3000 - dakika 7:32.23 (2001)
  • Mita 5000 - dakika 12:56.72(2001)
  • 10,000 mita - dakika 26:50.20 (2002)
  • Steeplechase mita 3000 - dakika 8:20.67 (1998)
  • Marathon - 2:06.43 (2007, muda: 2:06.45)

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Sporting positions
Alitanguliwa na
Moroko Brahim Lahlafi
Men's 5,000 m Best Year Performance
2001
Akafuatiwa na
Moroko Salah Hissou