Benjamin Limo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rekodi za medali
Men’s Wanariadha
World Championships
Dhahabu 2005 Helsinki 5000 m
Fedha 1999 Sevilla 5000 m

Benjamin Kipkoech Limo (alizaliwa 23 Agosti 1974 katika Chepkongony, Uasin Gishu) ni mkimbiajiwa umbali ya katikati kutoka Kenya . Yeye hukimbia kila umbali kutoka mita 1500 hadi mitA 10,000 , lakini hasa hushiriki katika mbio za umbali wa mita 5000 , ambapo yeye ameshinda medali za kimataifa.

Limo alienda shule za sekondari za Chebara na Lelboinet , lakini alijiunga na Jeshi la Kenya mwaka wa 1993, bila kumaliza masomo yake. Alianza mafunzo kwa ukamilifu mwaka wa 1996 na alikuwa na makao yake katika jeshi katika kambi ya Ngong, karibu na mji mkuu Nairobi. Yeye alishiriki katika mbio za kimataifa za nyika mjini Marrakech, Morocco mwaka wa 1998 na kumaliza wa nne katika mbio fupi. Hiyo ilikuwa shindano k\lake la kwanza nje ya nchi.

Medali yake ya kwanza ya kimataifa aliishinda mwaka wa 1999, wakati yeye alishinda mbio za nyika za dunia mwaka wa 1999 na kuwekwa katika nafasi ya pili katika mbio za mita 5000 katika mbio za dunia, sekunde moja nyuma ya Salah Hissou. Ona kwamba haya yaliyotokea mwaka mmoja baada ya mbio yake ya kwanza ya mita 5000 .

Mwaka wa 2002, Limo alishinda medali ya fedha katika Michezo ya Jumuiya ya Madola na katia mashindano ya Mabingwa wa Afrika. Katika mwezi wa Agosti 2005 alimshinda mbioSileshi Sihine na akawa bingwa wa ulimwengu. Yeye alishinda medali ya shaba katika mbio za mita 5000 mwaka wa katika mashindano ya Jumuiya ya madola.

Benjamin Limo hajawahi kushiriki katika Michezo ya Olimpiki, kutokana na kanuni ambayo inaruhusu wanariadha watatu tu kutoka kila taifa kushiriki. Taifa lake la Kenya lenye wingi wa wakimbiaji wema wengi wa umbali wa katikati, ni vigumu mno kwake kuhitimu.

Yeye alikimbia mbio refu mara ya kwanza mwezi wa Oktoba 2008 na kumaliza katika nafasi ya 12 katika mbio refu zaAmsterdam

Limo ilitunukiwa tuzo la mwanariadha bora mwanamume nchini kenya mwaka wa 2005 Yeye husimamiwa naRicky Simms wa Pace Sports Management.

Yeye ana mke na watoto wanne (kufikia mwaka wa 2006).

Limo hana uhusiano na bingwa wa dunia Richard Limo, lakini huenda ana uhusiano wa mbali na mkimbiaji mwingine wa Kenya, Felix Limo [1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. IAAF, 25 Agosti 2000: Si hata vipengele anaweza kuacha Jones Archived 18 Septemba 2004 at the Wayback Machine.


Sporting positions
Alitanguliwa na
Ethiopia Hailu Mekonnen
Men's 3,000 m Best Year Performance
2002
Akafuatiwa na
Moroko Hicham El Guerrouj


Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Benjamin Limo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.