Nenda kwa yaliyomo

Ray C.

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ray C)
Ray C
Ray C akiwa anatumbuiza
Ray C akiwa anatumbuiza
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Rehema Chalamila
Amezaliwa 15 Mei 1983 (1983-05-15) (umri 41)
Asili yake Iringa, Tanzania
Aina ya muziki R&B, Taarab, dansi, Bongo-bhangra
Kazi yake Mwimbaji
Ala Sauti
Miaka ya kazi 2002 mpaka leo
Ame/Wameshirikiana na Dknob, Chid Benz, Mh Temba, Squeezer, Nako 2 Nako
Tovuti MySpace


Rehema Chalamila (anafahamika zaidi kwa jina la kisanii kama Ray C; amezaliwa Iringa, Tanzania, 15 Mei 1982) ni mwimbaji wa muziki wa R&B, dansi, na bongo-bhangra kutoka nchini Tanzania.

Kabla ya kujihusisha na muziki, Ray C aliwahi kufanya kazi kama mtangazaji wa redio ya East Africa kabla ya kwenda redio ya Clouds FM ya jijini Dar es Salaam.

Mnamo mwaka 2003 alitoa Albamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la "Mapenzi Yangu".

Alianza kujulikana baada ya kutoa vibao kadhaa kama vile, Sikuhitaji, Mapenzi Yangu, Nawewe Milele, Ulinikataa na nyingine nyingi zilizompa umaarufu kama mwimbaji aliyeutingisha muziki wa Bongo Flava kati ya 2003-2009 — hadi hapo alipokuja kuingia matatani kiafya baada ya kutumia dawa za kulevya.

Mwaka wa 2012, Rais wa Tanzania wakati huo, Jakaya Kikwete, alitoa msaada mkubwa wa fedha kwa ajili ya matibabu ya Ray C na baada ya huduma mwimbaji huyu alikwenda kumshukuru kwa msaada wake.[1]

Mwaka wa 2016 imeripotiwa ya kwamba Ray C amerudi tabia yake ya kutumia dawa za kulevya, hali ambayo ilimkera sana Kikwete.

Albamu:

  • Mapenzi Yangu (2003)
  • Na Wewe Milele (2004)
  • Sogea Sogea (2006)
  • Touch Me (2008)

Mshindi:

Mshiriki:

  1. "Ray C kumtembelea Rais Kikwete Ikulu kwazua hisia tofauti - Bongo5.com", Bongo5.com (kwa American English), 2012-12-11, iliwekwa mnamo 2018-11-17
  2. Tanzania Music Awards - Winners 2004
  3. Tanzania Music Awards - Winner 2007 Archived 2010-07-10 at the Wayback Machine
  4. Musicuganda.com: PAM 2006 nominees Archived 2010-05-22 at the Wayback Machine
  5. PAM Awards
  6. allAfrica.com: '20 Percent' Grabs Seven Kili Music Awards Nominations

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
  • Ray C katika Tanzania Directoty.info
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ray C. kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.