Nenda kwa yaliyomo

Nako 2 Nako

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kutoka kushoto ni Bou Nako, Ibra da Hustler, Lord Eyez na G Nako aka G-warawara

Nako 2 Nako (Nako to Nako, N2N au Nako 2 Nako Soldiers) ni kundi la hip hop kutoka Kaskazini mwa Tanzania - Arusha. Kundi linaundwa na wanachama wanne (4) ambao ni Lord Eyez, G Nako, Ibra da Hustler na Bou Nako. Msanii Ibra da Hustler alijitoa kwenye kundi mwez wa 11, mwaka 2008 kutokana na kupishana maelewano na wanamuziki wenzake kwenye kundi. Hivyo, Ibra da Hustler anaendelea kufanya muziki wake mwenyewe pasipo kua na kundi (solo artist). Jina la nako 2 nako lipatikana katika gym ya mazoezi (maarufu kama dojo) ambayo iliwakutanisha wanamziki hawa wakiwa wanafanya mazoezi. Kundi hili pia linaundwa na wasani wengine ambao bado hawajapata umaarufu sana (Junior nakos) pamoja na wanakikundi wengine wasio wanamziki, yaani jumuia ya wanamazoezi wa gym ambayo mazoezi ya dojo yalikua yakifanyika.

Kwa muda mrefu kundi hili limeonyesha uwezo mkubwa katika kuwakilisha muziki wa kizazi kipya aina ya rap au hiphop. Nako 2 Nako wamepata umaarufu kwa ustadi wao wa kughani kwa kutumia Lugha ya Kiswahili.

Baadhi ya nyimbo zao maarufu[hariri | hariri chanzo]

Na bado tunazidi

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nako 2 Nako kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.