Rasi ya Kola

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rasi ya Kola katika Urusi
Rasi ya Kola kati ya Bahari ya Barents (kaskazini) na Bahari Nyeupe
Bandari ya Murmansk
Ziwa la Imandra, nyuma milima ya Chibiny
Bweha aktiki ana rangi inayolingana na theluji

Rasi ya Kola (kwa Kirusi Ко́льский полуо́стров kolsky poluostrov) ni rasi iliyoko kaskazini magharibi mwa Urusi. Sehemu kubwa ya maeneo ya Obmansk Oblast iko humo. [1] Eneo la rasi ni km2 100000, linganisha Murmansk Oblast jumla km2 144900.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Rasi iko kabisa ndani ya mzingo aktiki ikipakana na Bahari ya Barents upande wa kaskazini na Bahari Nyeupe pande za mashariki na kusini-mashariki. Jiji la Murmansk ndilo mji mkubwa wenye wakazi zaidi ya 300,000 ambao ni wengi kwenye rasi.

Rasi hii ni baridi mno kwa kilimo ilikaliwa na wawindaji na Wasami waliofuga kulungu aktiki (reindeer). Tangu karne ya 12 Warusi kutoka Novgorod walianza kufika na rasi ilikuwa chini ya mamlaka ya milki za Warusi. Walivutwa na bahari yenye uvuvi bora; ingawa Kola iko upande wa kaskazini wa mzingo aktiki, bahari yake haina barafu ya kudumu kwa sababu mkondo wa ghuba kutoka Atlantiki unaendelea kupeleka maji ya vuguvugu hadi huko. Katika maji hayo samaki mbalimbali wanapatikana kwa wingi.

Katika kipindi cha Umoja wa Kisovyeti uchimbaji wa madini ulipanuka pamoja na tasnia za uvuvi na ufugaji wa kulungu aktiki. Idadi ya wakazi iliongezeka sana.

Bandari za rasi zilikuwa vituo muhimu kwa wanamaji wa jeshi la Kisovyeti. Bandari kuu ni Murmansk.

Baada ya kufsambaratika kwa Umoja wa Kisovieti, uchumi ulirudi nyuma na idadi ya watu ikaanza kupungua haraka. Kati ya 1989 na 2002, Obmansk Oblast ilipoteza karibu robo ya wakazi wake. Lakini uchumi uliibuka kwa kiasi fulani katika muongo wa kwanza wa miaka ya 2000 na rasi bado ndio eneo linaloonyesha maendeleo kati ya miji ya kaskazini ya Urusi.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. 2007 Atlas of Murmansk Oblast, p. 2

Marejo mengine[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Urusi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Rasi ya Kola kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.