Rashid Chidi Gumbo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rashid Chidi Gumbo
Maelezo binafsi
Tarehe ya kuzaliwa 14 Oktoba 1988
Mahala pa kuzaliwa    Dar es Salaam, Tanzania
Urefu 1.70 m
Nafasi anayochezea Kiungo wa kati
Timu ya taifa
Timu ya Taifa ya Tanzania

* Magoli alioshinda

Rashid Chidi Gumbo (alizaliwa 14 Oktoba 1988), alikuwa mchezaji wa mpira wa miguu wa nchini Tanzania, ambaye alicheza kama kiungo wa kati. Alichezea vilabu mbalimabli nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na Mtibwa Sugar F.C., African Lyon F.C., Singida United F.C., Simba S.C. na Young Africans S.C..[1]

Ushiriki Kimataifa[hariri | hariri chanzo]

Alicheza mchezo wake wa kwanza wa kimataifa katika Timu ya Taifa ya Tanzania dhidi ya Timu ya Taifa ya Rwanda mnamo Agosti 2009. Mchezo huo ulichezwa katika uwanja wa Stade Amahoro jijini Kigali, Rwanda. Gumbo alifunga bao la kufutia machozi katika mchezo huo uliomalizika kwa 1-2. Pia alishiriki mechi mbalimbali katika mashindano ya kimataifa ikiwa ni pamoja na michuona ya kombe la CECAFA 2011, ambapo Timu ya Taifa ya Tanzania ilipata ushindi wa bao 1 - 0 dhidi ya Timu ya Taifa ya Malawi kwenye nusu fainali ya michuano ya kombe hilo.[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Benjamin Strack-Zimmermann. "Rashid Gumbo (Player)". www.national-football-teams.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-03-12. 
  2. Benjamin Strack-Zimmermann. "CECAFA Cup (2011) | Final Tournament | Quarter Finals". www.national-football-teams.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-03-12. 
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rashid Chidi Gumbo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.