Singida United F.C.
|
Singida United ni klabu ya soka inayocheza Ligi Kuu Tanzania Bara yenye makao yake huko Singida. Wanatumia uwanja wa Namfua uliopo Singida kwa mechi zake za nyumbani. Katika ligi daraja la pili, Singida United walishinda taji hilo kwa mara ya pili mfululizo mwaka 2016, walishinda pia taji la ligi daraja la kwanza mwaka 2017.
Mnamo Januari 12, 2019, Mserbia Dragan Popadic alichaguliwa kuwa kocha mkuu na msaidizi wake kua Dusan Momcilovic.[1]
Historia
[hariri | hariri chanzo]Singida united ilianzishwa mkoani Singida kanda ya Tanzania kati mwaka 1972 miaka hiyo ikijulikana kama Mto Sports Club [2]. ilianza kama klabu ndogo na baadae kuanza kuvutia wadau katika miaka ya 90. Kwa mara ya kwanza, Singida united ilishiriki ligi kuu Tanzania bara mwaka 2000. Hawakua na mwanzo m,zuri kwani walishuka daraja msimu unaofuata wa 2001/2002. Ilishiriki ligi daraja la kwanza kwa muda mrefu na ikashuka mpaka ligi daraja la pili, kuanzia mwaka 2013, Singida united ilirudi katika kiwango bora, iakapanda mpaka daraja la kwanza amabapo iliendelea kufanya vizuri kwa misimu kadhaa.
Hatimaye mwaka 2017, klabu hiyo ilipanda hadi Ligi kuu Tanzania Bara kitendo kilichopelekea wadhamini wengi kujitokeza kuidhamini klabu hiyo. Klabu hiyo ilipata udhamini wa kampuni ya sportPesa ikiwa ndio mwaka wa kwanza wa kampuni hyo kuingia nchini Tanzania, kuacha udhamini huu wa kamopuni ya kubashiri, Singida united ilipata udhamini wa Puma pia, kampuni ya nishati Tanzania.[3]
Msimu wa 2018/19
[hariri | hariri chanzo]Katika msimu wa 2018/2019, ndai ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Singida united nilicheza jumla ya michezo 38, ikishinda michezo 11, sare 13 na kupoteza michezo14, ilimaliza katika nafasi ya 13 ikiwa na jumla ya alama 46.[4] Katika mashindano ya Azam Sports Federation Cup, walifika hatua ya robo fainali kabla ya kupoteza mchezo kwa idadi ya magoli 2–0 dhidi ya Lipuli FC.
Mafanikio
[hariri | hariri chanzo]- 2016 Ligi Daraja la kwanza Washindi wa Kundi C
- 2017 Ligi Daraja la Pili Washindi wa Kundi A
Kikosi cha sasa 2018/19
[hariri | hariri chanzo]Note: Flags indicate national team as has been defined under FIFA eligibility rules. Players may hold more than one non-FIFA nationality.
|
|
Benchi la Ufundi
[hariri | hariri chanzo]Wasimamizi
[hariri | hariri chanzo]- Dragan Popadic (2019–mpaka sasa)
- Hemed Seleman Ally 'Morocco' (2018–2019)
- Hans van der Pluijm (2017–2018)[5]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Singida United appoint former Express FC coach". swiftsportsug.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-05-30. Iliwekwa mnamo 2019-05-30.
- ↑ "Singida Utd Team History". SportPesa Care Facebook Page (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-05-30.
- ↑ "Singida United yazidi kutajirika", Mwanaspoti. Retrieved on 2019-10-01. (en-UK) Archived from the original on 2019-10-01.
- ↑ "Tables – LIGI KUU BARA". (en)
- ↑ "Hans van der Pluijm appointed head coach of newly-promoted Tanzanian side Singida United". GHANAsoccernet.com. Iliwekwa mnamo 2017-07-26.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Singida United Facebook page (Kiingereza) na (Kiswahili)
- Singida United Twitter page
- Singida United Instagram page
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Singida United F.C. kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |