Nenda kwa yaliyomo

Uwanja wa michezo wa Amahoro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uwanja wa Michezo Amahoro

Uwanja wa michezo wa Amahoro pia hujulikana kama Uwanja wa Taifa wa Amahoro ni uwanja wenye shughuli mbalimbali za kimichezo huko Gasabo, Kigali nchini Rwanda. Una uwezo wa kuhimili watu takribani elfu 25,000, ni uwanja mkubwa zaidi nchini Rwanda na huandaa mechi za mpira wa miguu, matamasha, na hafla mbalimbali za umma. Vilabu vya mpira wa miguu kama Armée Patriotique Rwandaise F.C. na Rayon Sports F.C vimepanga katika uwanja huo. Uwanja pia wakati mwingine hutumiwa kwa michezo ya ragi.

Wakati wa mauaji ya kimbari ya Rwanda mnamo mwaka 1994, ulilindwa kwa muda na Umoja wa Mataifa na kuhudumia hadi wakimbizi 12,000, haswa Watutsi.

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Amahoro kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.