Rafaeli Guizar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rafaeli Guizar

Rafaeli Guízar Valencia
Amezaliwa
26 Aprili 1878
Nchi Mji wa Mexiko
Kazi yake askofu mkuu
Kaburi la Mt. Rafaeli Guízar Valencia huko Jalapa.

Rafaeli Guizar (Cotija, Meksiko, 26 Aprili 1878 - Mji wa Meksiko, 6 Juni 1938) alikuwa askofu mkuu wa Veracruz-Jalapa kuanzia mwaka 1919.

Kwa kuwa alijihusisha na vita vya Cristeros aliondolewa jimboni mwake ikambidi aishi na kuendelea na uchungaji wake mafichoni jijini Mji wa Meksiko hadi kifo chake.

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 29 Januari 1995, halafu Papa Benedikto XVI alimtangaza mtakatifu tarehe 15 Oktoba 2006.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[1].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.