Nenda kwa yaliyomo

Qanbalu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Qanbalu (pia Kanbalu, kwa Kiarabu قنبلاو) ni jina la kihistoria kwenye pwani ya Afrika Mashariki linalotajwa katika maandiko ya waandishi Waarabu wa karne za kati.

Mara nyingi hutazamwa kama jina la zamani la Kisiwa cha Pemba (Tanzania)[1] au hasa kwa mji ambao maghofu yake hupatikana kwenye Ras Mkumbuu kwenye kisiwa hicho[2] .

Zamani, na hasa kwa waandishi Wafaransa, jina la Qanbalu lilitafsiriwa pia kwa maana ya Madagaska[3].

Mpelelezi na mwanahistoria Mwarabu Al-Masudi aliandika mnamo mwaka 900 "Mabaharia wa Omani wanasafiri kwenye bahari hii (yaani Bahari ya Ethiopia au Bahari Hindi) hadi kisiwa cha Kanbalu kilichopo katika bahari ya Zanj. Kisiwa hukaliwa na Waislamu na Wazanj ambao hawakupokea Uislamu.[4] "

Qanbalu ya Al Masudi ilikuwa kituo muhimu kwenye njia ya kuelekea Sofala iliyokuwa mwisho upande wa kusini kwenye safari za Bahari Hindi na bandari ya dhahabu kutoka Ufalme wa Mutapa (Zimbabwe) iliyopelekwa hadi Uarabuni na Uhindi.

  1. Reid, Lane: African Historical Archaeologies (2014) (kupitia google books), p. 135f
  2. Oliver, Oliver & Fagan: Africa in the Iron Age: C.500 BC-1400 AD (1975) (kupitia google books) , p. 193f Hao wanasema ya kwamba Ras Mkumbuu imethibitishwa kuwa sawa na Qanbalu, lakini wengine hawakubali
  3. linganisha Ed. Dulaurier, Les Sciences arabes au moyen-âge (1851), kupitia fr.wikisource.org
  4. Al-Masudi: Meadows of Gold and Mines of Gems, an English translation of the Muruj al-dhahab by Aloys Sprenger, London 1841 (google books), uk. 232,260