Maghofu ya Ras Mkumbuu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Coordinates: 5°13′00″S 39°40′00″E / 5.21667°S 39.66667°E / -5.21667; 39.66667


Mahali pa Ras Mkumbuu kwqenye kisiwa cha Pemba

Maghofu ya Ras Mkumbuu yanapatikana kwenye pwani ya magharibi ya kisiwa cha Pemba (Tanzania). Yapo karibu na kijiji cha Ndagoni mwishoni mwa rasi ndefu nyembamba inayojulikana kama Ras Mkumbuu iliyopo upande wa kaskazini magharibi mwa mji wa Chake Chake.

Kutokana na utafiti wa kiakiolojia maghofu yanatokana katika kipindi cha karne ya 13 na 14, ingawa kuna dalili kwamba yalijengwa juu ya misingi ya kale zaidi. Miongoni mwa maghofu haya kuna msikiti mkubwa.

Mwanakiolojia James Kirkman aliyekuwa wa kwanza kuchimba hapa katika miaka ya 1950, alipendekeza kuona maghofu haya ni mabaki ya "Qanbalu" (pia: Kanbalu, kwa Kiarabu: قنبلاو) iliyotajwa na mpelelezi Mwarabu Al-Masudi mnamo mwaka 900 BK[1] lakini hakuweza kutambua mabaki ya zamani kuliko karne ya 13 [2] .

Wataalamu bado wanajadiliana kama "Qanbalu" ya Al Masudi ilikuwa kisiwa cha Pemba kwa ujumla na labda hasa mahali pa maghofu ya Ras Mkumbuu [3] .

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Al-Masudi: Meadows of Gold and Mines of Gems, an English translation of the Muruj al-dhahab by Aloys Sprenger, London 1841 (google books), uk. 232,260
  2. Reid, Lane: African Historical Archaeologies (2014) (kupitia google books), p. 135f
  3. Oliver, Oliver & Fagan: Africa in the Iron Age: C.500 BC-1400 AD (1975) (kupitia google books) , p. 193f Hao wanasema ya kwamba Ras Mkumbuu imethibitishwa kuwa sawa na Qanbalu, lakini wengine hawakubali

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Finke, J. (2006) The Rough Guide to Zanzibar (2nd edition). New York: Rough Guides.