Sofala

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Picha ya kuchora ya Sofala mwaka 1683

Sofala (leo hii: Nova Sofala) ni bandari na mji mdogo katika Msumbiji karibu na mji mkubwa wa Beira. Uko kando la mdomo wa mto Sofala unapoishia katika Bahari Hindi.

Tangu kuundwa kwa Beira Sofala haina umuhimu tena lakini ilikuwa bandari kuu ya Msumbiji wote kwa karne kadhaa kabla ya kuja kwa Wareno.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Sofala ilikuwa bandari ya biashara ya dhahabu jutoka milki ya Mwene Mtapa. Vilevile ilikuwa bandari ya kusini kabisa kati ya mabandari ya Afrika ya Mashariki ambako wanfanyabiashara Waswahili na Waarabu walifika mara kwa mara.

Taarifa ya karne ya 17 ya msafiri Mfaransa Vincent Leblanc yasema kuwa mji wa "Cefala" uliundwa na Waislamu kutoka Kilwa na Mogadishu akitaja pia migodi ya dhahabu za Manika katika Zimbabwe ya leo. Inaaminiwa kuundwa kwa mji kulitokea katika karne ya 9 BK.

Wareno walitwaa Sofala na mwaka 1505 walijenga boma muhimu kama kituo cha kijeshi alipokaa gavana wa kwanza wa Wareno katika Msumbiji. Bandari yake iliweza kutunza jahazi 100. Tangu kuhamishwa kwa makao makuu kwende Msumbiji kisiwani umuhimu wa mji ulipungua na baada ya kuundwa kwa Beira mwaka 1871 ulipotea kabisa.

Mawe ya boma lake yaliondolewa na kupelekwa Beira kwa ujenzi ka Kanisa Kuu jipya.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]